Monday, September 19, 2011

TUONGELEE FAMILIA...

sijui vitabu vya dini vya kiislamu vinasemaje lakini najua vitabu vya dini vya kikristo vinasema ya kwamba MUNGU alimuumba mwanaume na kwa kumtazama akaona japo mwanaume alipewa kila kitu hakuwa na raha na vitu vile ndio MUNGU akamuumba mwanamke kutokana na ubavu wa mwanaume. biblia ndio isemavyo..

sasa basi najiuliza kweli kila ndoa iliyofungwa watu hao ni mtu na ubavu wake????? na kama ni hivyo kwanini ndoa huvunjika na baadaye mtu kuoa ama kuolewa na mtu mwengine???? ama sisi tunafanya tofauti na mapenzi ya MUNGU viherehere vyetu vya kutaka kuoa na kuolewa vinatupelekea kutokupata ubavu wetu kwa sababu ya haraka zetu????

je wewe uliye na ndoa sisemi kwamba kila mwenye ndoa hakupata ubavu wake lakini najuwa ndoaa yingi tu zinafuraha, upendo na amani tele, yani watu wanafurahia kuoana kwao na kila siku kwao ni baraka hata kama malumbano ya hapa na pale yapo(kwani hili ni jambo la kawaida) wao wala utawakua na furaha kutwa hawana vinyongo..

 Lakini utakuta kwenye ndoa nyengine mwanaume mzima eti anamchunia mke wale hata wiki mbili au hata tatu haongei naye akiingia kama upepo akitoka kama upepo sasa unajiuliza ndoa ile mwanamke nani na mwanaume nani maana mambo ya kuchuna ni mambo ya mwanamke sasa mwanaume akichuna inakuwaje???


unywaji wa pombe kiholela nayo husababisha ndoa nyingi sana kuvunjika, hivi wewe mama ama wewe baba kunywa pombe ni kitu cha kawaida lakini na shangaa mtu mwengine anakunywa sasa ile starehe yake inakuwa kero kwa mkewe/mumewe na hata majirani, watu wengine yani nahisi wanajilazimisha tu kulewa nao waonekane hawajapitwa na wakati,mara umelewa ndio mpaka unasinzia bar wenzio wakubebe urudishwe nyumbani ukifika unakuwa mzigo kwa mkeo ama mumeo maana kero tupu utakuta wengine wanatapika, mwengine ndio hata chooni kwenda hawezi anajimalizia hapohapo, mwengine kulala hawezi anazunguka tu kwenye kitanda kama pia, yaanii...

 utamkuta mwengine anakaa kwenye bar mpaka saaa saba za usiku mara mkeo hamu imempanda anafanyaje ama ndio yale anajimalizia mwenyewe huku anamfikiria mwanaume (akimfikiria mwanaume mwengine na sio wewe mumewe inakuwaje, hii ikitokea mara nyingi unakuta yule mama hamu tena ya mapenzi na mumewe anakuwa hana)..

kingine nilichokiona kinaharibu sana familia utakuta mwanaume ama mwanamke kutwa kiguu na njia utadhani umekula miguu ya kuku, mtu hutulii kwako, ukajuwa familia yako imekaaje wiki nzima, watoto wanaendeleaje kama wanaenda shule wanaendeleaje kimasomo, ama hata uwatoe out week end na wenyewe wakaenjoy sio kila siku wako ndani kama kuku anayelalia mayai yake kutwa kayalalia..

utakuta wengine hata hawajui siku ya kuzaliwa mkewe ama mumewe, maana hamna mapendo cha muhimu mtu kala, kavaa nguo safi na akitaka mzigi abebe basi, ndoa hapa itakuwa ndoa ama kifungo, ndio maana wengi siku hizi sio waaminifu, na ndio maana ndoa nyingi zinavunjika na wanaopata shida ni watoto..

kwasababu kama mtu hupati ndani inamaana ukapate wapi? sisi wenyewe ndio wenye uwezo wa kubomoa na kujenga nyumba zetu na ndoa zetu lakini mnapojaribu na kuona inashindikana basi ni afadhali ya kuachana msijee kuuna na magonjwa,  maisha yenyewe haya tunaishi mara moja ukifa umekufa hutarudi tena kama wewe labda ukirudi tena kutakuwa hamana kuoa ama kuolewa.

familia ni jambo la kheri, wengi mtaani wanatamani kuwa nayo lakini bahati hiyo hawakupata na wengine mpaka kuzeeka bila kuipata, basi ukiwa nayo uwe na ndoa ama unawatoto tu basi tujitahidi kuipenda na kuilea kwa kumtegemea na kwa hofu ya MUNGU.




1 comment: