Rose,
mwenzio nacheka kwa uchungu, niliolewa mume wangu baada ya miaka sita ya ndoa yetu mume wangu akanitaarifu ya kwamba anataka kuoa mke wa pili, japo iliniuma sikushangaa sana kwani dini yetu inaruhusu kuoa wake hata wanne ikiwa tu utaomba ruhusa kwa mke wa kwanza naye akaridhia, basi kwakuwa mume wangu alisharidhia kuoa na kampata wa kumuoa sikuona kwanini nimkatalie nikamwambia amwambie tu huyu mkewe akija tuheshimiane na kila mtu ajuwe mipaka yake.
basi mume wangu yule akaanda harusi siku ikafika kweli akaoa, na siku ya harusi mke mwenzangu kweli alipendeza na kutunzwa zawadi tele, ndugu zake wa kitanga nakwambia wakajipamba taarabu zikapigwa lakini cha kushangaza taarabu zile kama zilikuwa zinanisema miye kwa mafumbo maana nyingi zilikuwa za kuhusu uke wenza, na mwanaume kwenda kwake nikaanza kuhisi kimchezo.
kwasababu ile harusi ya mume wangu nami na wakwe na ndugu wa mume wangu wote tulikuwa mstari wa mbele kuifanya ifane lakini wale ndugu wa mwanamke na yule aliyeolewa nikawa naona kama vile wameichukulia dili sana miye kuletewa mke mwenzangu yani kama vile sijui nini..
yule dada akagewa naye nyumba yake huko boko, maisha yakawa yanaendelea lakini kwa masimango akinisema vibaya kwa watu kwamba sifai wala simtimizii mume wangu ndio maana kaolewa yeye, kila nikipita kwa ndugu wa mume wangu napewa tu habari alizopeleka kuhusu mimi na kunisingizia vitu kibao, wakati miye nilikuwa namsalimia na kumjulia hali kila mara mume wangu akienda nikinunua chochote hata kanga namgea na yeye lakini yeye anilipiza kwa masimango na kunisema najipendekeza, wakati nilimruhusu mwenyewe mume wangu amuoe leo nasemwa kamfwata yeye sijui kutunza mume!!!!!!!!
wamekaa miaka miwili hivi yule dada hajashika mimba mpaka wakaanza kuzunguka kwa waganga, na madawa yote ya kienyeji yakamalizwa lakini wapi kumbe mwenzangu yule dada alikuwa anatumia dawa za majira ili asizae na mumewe hajui kumbe kawaida yake huwa anajiuza kwenye mahoteli makubwa na ndio huko alipokutania na mume wangu.
ikafika sasa mpaka nikaambiwa namloga ili asizae, akaanza kuniongelea vibaya mpaka kwa mume wangu, mume wangu na yeye kwa kupenda ya kuambiwa akanibadilikia kutwa akawa analala kwa mke mdogo kwangu kapasusa hela ya matumizi hanipi tena ananiambia nipewe na hao wanaume wangu yani vituko kibao na akaamua kuhamia kwa bimdogo.
ikabidi tena nitafute mtaji nianze kufanya biashara za hapa na pale namshukuru MOLA maisha yanaendelea, yule mume wangu ndio kaganda kwa mke mdogo hata kuja kusalimia wanae haji wala matumizi haleti.
yule mke mwenzangu yapo alikuwa na ndoa alikuwa anakutana na majamaa zake kwa siri, mwaka wa tatu MUNGU akamjalia akapata mimba, akaanza kwenda clinic na siku akatakiwa kupima ukimwi majibu yakaja amehathirika, akachanganyikiwa atafanyaje??? akawaeleza dada zake waliokuwa wanajuwa siri zake wakamwambia sasa kashaumbuka atafanya nini zaidi aje kuniona mimi aniambie nimpe ushauri.
akaja na dada zake watatu, nilishangaa nikajuwa anataka kuja kunifanyia vurugu, akanieleza kwa upole akitokwa na machozi kwa uchungu, nikaona kama mchezo wa kuigiza japo kanifanyia mengi mabaya na kunitia ubaya kwa watu nilimuonea huruma sana, ni ka mwambia sawa nitamsaidia na kumsaidia kwangu ni kwamba amueleze mumewe ukweli japo anaweza kupigwa na kuumizwa lakini atakuwa kashajuwa na yule baba akija huku miye nitamuelewesha kwamba asiwe na jazba.
mumewe aliporudi siku hiyo akamueleza mambo yote, kweli yule baba alipandwa na hasira sana sema akashindwa kumpiga kwasababu alikuwa mjamzito, kama tulivyojuwa mume wangu akaondoka na kuja kwangu kwasababu nilikuwa nimeshajuwa nikamruhusu tu kuingia ndani japo nami nina dukuduku langu.
baada ya kula na kuoga nikamuuliza vipi leo umekosea njia, ndio akaanza kuniomba msamaha akitokwa na machozi kisha akanihadithia yote, sikumjulisha kwamba nilikuwa najuwa, nilichomwambia ni kwanza omba wanao msamaha kisha asubuhi twende hospital tukapime maana wote tunaweza tukawa tumeambukizwa.
kesho yake tukaenda, tukapima kwakweli hatukuamini tulivyokuta wote wawili hatuna maabukizo, japo tulifurahi lakini hatukuamini, kwangu niliamini kwani mume wangu aliniacha na sikuwa na mtu mwengine tena ila yeye hakuamini kwani mkewe alikuwa nao halafu yeye hana hakuelewa kabisa, tukaambiwa tupime tena baada ya miezi mitatu, tukapima na kweli hatuna.
yule mke mwenzangu akajifungua mtoto ikawa bahati mbaya amefariki, ikabidi baada ya kupona mume wangu ampe talaka akarudi nyumbani na kunieleza jambo moja SITAKAA KUKUACHA TENA.
nimeandika leo ili kumshukuru MOLA wangu kwa kunirudishia familia yangu, na kuwapa moyo wanawake wote ndoa zao zenye matatizo kwamba MOLA ni mwema atamrekebisha mumeo kwa njia yake mwenyewe na kwa muda wake mwenyewe jipe moyo na endelea kuvumilia.
pole sana dada hii kama film vile bonge ya stori dada ni kumrudishia mola utukufu umshukuru sio tu kwavile amekurudishia famila yako pia amekuepusha na ugonjwa hatari la ukimwi
ReplyDeletepole dada na hongera mumeo kurudi. mumeo ajifunze umalaya sio mzuri. atulie na mke mmoja inatosha. na hizo dini zenu nazo hovyo... zinasababisha muambukizane ukimwi
ReplyDeletePole dada kwa majaribu. Ila mshukuru Mungu sana kwani anakupenda saaana. Hata kama dini zinaruhusu wake wengi tujue kuwa hawa waume zetu wakati mwingine wanaenda kuleta vyangu doa ndani kisa dini inaruhusu. Ili liwe funzo. Hata kama unaoa wa pili basi awe dada na heshima zake si kuokoteza malaya
ReplyDeleteduh, Pole sana sana mamii, Mungu awe kiongozi wa familia yako...yan nimesisimka naona kama movie vile.
ReplyDelete