leo kuna mkasa mmoja ambao nimeusikia kwakweli umenishangaza, kuna dada mmoja ambaye kwa muda mrefu sana amekuwa akitafuta ajira hapa jijini bila mafanikio yoyote na sio kwamba alikuwa hana vyeti vya kuridhisha bali tu labda bahati hakuwa nayo maana wote tunajuwa haichukui vyeti tu kupata kazi haswa kwa wakati huu..
dada huyu alikuwa ameolewa na yupo kwenye ndoa kama mwaka sasa na kipindi hicho ndio walikuwa wamebahatika kupata mtoto yani alikuwa mjamzito, na kweli wanasema kila mtoto huja na bahati yake na kipindi hicho huyo dada akawa ameitwa kwenye interivew ya kazi kweli akafanya na akapata kazi sasa kimbembe kinakuja yeye ni mjamzito na kazini atafanyaje miezi tisa na kuondoka kulea mimba kitu hicho wale waajiri wake hawajakitaka kabisa..
basi dada huyu ikabidi atoe ile mimba ya miezi miwili ili adumu kazini, jamani huu ni unyama hatakama maisha ni yake kweli wakati huu tunaweza kuruhusu pesa kutoa uhai wa mtu, mume wake sasa amechanganyikiwa na kushangaa mke wake mimba hana tena, anahasira sana mke kama huyu utamfanyaje ukimrudisha kwao itakuwa vibaya??????????????
Pesa ni kitu kishenzi sana. Mungu amsamehe.
ReplyDeleteIlo tatizo ni kubwa tusiliangalie juu juu. Nadhani hata kwenye ndoa kulikuwa hakuna mawasiliano; huwezi toa mimba tena ya mtoto wa kwanza bila kumshirikisha mumeo nadhani ndoa yao itakuwa ina ugomvi ila watu hamwezi kujua. Pili nadhani Bunge liingilie kati haya masuala ya waajiri kukataa mtu sababu ya mimba. Najua hairuhusiwi ila waajiri wanafanya ujanja wa kupima watu kabla ya kuwapa ajira. Iwe ni marufuku kupima afya ya mtu wakati wa ajira kwa kuwa wanatumia vibaya matokeo ya vipimo. Huo ni ubaguzi wa kijinsia.
ReplyDeleteNarudia tena yawezekana kabisa hiyo ndoa ni shubiri huwezi kuua mtoto wako wa ndoa tena huna mwingine na hujuhi kama Mungu atakupa tena kwa sababu ya kupenda sijuhi kazi au pesa