Saturday, May 28, 2011

HAIPENDEZI UKIWA UNANUKA JASHO HASWA KWENYE MARAHA....

jamani tukubali tukatae jasho linakera jamani, unajuwa kuna jasho lengine linaraha na lengine lina tia kichefuchefu haswa pale mnapokuwa kwenye maraha yenu chumbani...


kila binadamu aliumbwa na kutokwa jasho lakini majasho hutofautiana wengine hutokwa na mengi na wengine hutokwa na kidogo na haya yote husababisha mpaka kunuka haswa lile jasho la kwapa na hapa utakuta mtu anakikwapa kikali sana na wala hana wasiwasi nacho...


sawa ni chako lakini hebu tuangalie pale tunapokuwa faragha na mwenzetu maana pale wengine ndio jasho linawatoka haswa na kama mambo ya manukato huyajui basi balaa tupu, leo nataka niseme sio vibaya mtu kutokwa na jasho jingi ama linalotoa harufu lakini nataka kuwashauri kwa wale wanaonuka jasho mkiwa kwenye maandalizi ya maraha oga paka manukato haswa yale yenye harufu kali kidogo ili iweze kukata ile harufu usimkere mwenzako...


na maranyingi mtu jasho la kwapa huwa baya zaidi kwasababu ya kutojifanyia usafi kisawasawa yani kunyoa nywele za makwapa hizo ndizo zinazofanya jasho liwe balaa kwako, na kujisafisha vizuri hebu tuchukuwe muda wa kujisafisha vizuri kila idara tuepuke kunuka na kujitia aibu...


utamkuta dada bomba lakini ukimsogelea karibu unahisi kutapika anavyonuka jasho ama utamkuta kaka kavalia anaonekana mtanashati lakini weeee muache akukuruke kidogo uone kijasho kinavyotema..... haipendezi

1 comment:

  1. Hii inanikumbusha wale wanaume ambao wakati wa sex majasho yanawamiminika na yote yanakumwagikia kwenye uso, macho, mdomo etc. Halafu hata hapangusi maana yeye anaendelea tu na kazi....jamani hata kama uroda ni muhimu lakini unaweza kuchukua break na kufuta jasho na kuendelea.

    ReplyDelete