Sunday, April 24, 2011

TOFAUTISHA KATI YA RAFIKI NA MPENZI...



Leo nataka kuzungumzia hili jambo ambalo nimeliona sana likitendeka kwenye jamii, hivi umeshawahi kujiuliza mpenzi wako ni rafiki yako ama rafiki yako ni mpenzi wako?????


Maana bwana haswa nataka kuzungumzia upande wa kina dada maana hawa ndio haswa nimeona wenye matatizo kwenye hili jambo, wasichana wengi hawajui kutofautisha kati ya rafiki na mpenzi na ndio maana wasichana wengi hutukanwa na wanaume kuwadhani ni malaya...


Wanawake nimegundua baadhi wanatabia wanapoongea na mwanaume ambae sio mpenzi wake utakuta mdada anajichekesha sana bila hata aibu mara amshike mwanaume mkono, mara aanze kumsifia mara oohhh twende nikakupe bia leo inahusu jamani..... unajitongozesha!!!! mara akikugusa kidogo unataka uguswe tena mara mnaishia gesti unaenda kuliwa halafu unaachwa kwenye mataa....haipendezi


Baadhi ya wanawake wanashindwa kabisa kujiheshimu halafu hawajui kama wanaume hawa wanaojichekesha kwao wakitoka hapo wanaenda kuhadithiana kwamba yule hamna lolote hata wewe ukitaka utampata, atakuja na mwengine atajifanya kakuzoea na baadae mambo yanakuwa yaleyale.... tujifunze kujiheshimu....



Ama utakuta mwanamke ama mwanamme anamuita rafiki kwa jina la mpenzi, sweety, honey japo haimaanishi kwamba uponaye kimapenzi lakini hii lugha sio nzuri haswa pale mke,mume ama mpenzi wako anaposikia ukimuita mtu mwengine haswa wa jinsia tofauti, hapo ndipo anapoanza kuwa na mashaka na wewe...


tujue kutofautisha kama rafiki yako muite kwa jina lake usimuudhi mpenzi wako na acha kujirahisisha na kujichekesha utaliwa na kuachwa na wangapi unakuwa shimo la taka kila zagazaga zinaingia!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment