Friday, April 29, 2011

KABUNI NAMBA NA KUNITONGOZA....



tabia hizi za kubuni namba jamani zimetoka wapi???? ama kwasababu sikuhizi bei chee kupiga simu!!!!!! yani we mtu unajikuta unabuni tu namba na kupiga kweli watu sikuhizi wanatumia simu vibaya na hivi zinauzwa kwa bei rahisi mbona tutakoma kusumbuliwa....


kuna kaka mmoja hivi kama miezi miwili sasa tokea nimeongea naye kwa mara ya kwanza, akanipigia simu mara baada ya kuongea naye akaniambia samahani nimekosea namba lakini kwasababu ya ukarimu wako na kuongea na mimi vizuri naomba japo niwe nakupigia nikujulie ghali....



sikuona kama ni mbaya nikamkubalia kwani salamu itanifanya nini??? mara kila wiki akawa anapiga na kunisalimia mara akaanza kuniambia mambo yake story zikawa nyingi nikawa namshauri tukaendelea nikimchukulia tu kama rafiki wa kawaida kwani sikuwa na wazo naye lolote mara baadae akajakuanza ohhh ninafurahi sana ninavyoongea na wewe unanipa faraja mara alipojuwa sina mtu akaamua kunitongoza....kwakweli nilishangaa sana..




sawa sikatai kwamba kwa simu anaonekana ni kijana wa maana, lakini ninachojiuliza kama amefanya hivyo kwangu namba ngapi atakuwa amebuni na kuwatongoza, kwasababu sijamjibu yaani ananisumbua mpaka natamani kubadilisha line, marafiki zangu wananiambia nimpe muda kwani siwezi juwa MUNGU alichonipangia labda ndio mume wangu...




lakini jamani huku si kujidhalilisha hivi kweli mtu anaweza kukutaka wakati hajawahi hata kukuona kasikia sauti tu.....

1 comment:

  1. DADA UNASEMA UNASUMBULIWA NA KAKA ALIYEBUNI NAMBA YA SIMU NA KUKUPIGIA NA SASA ANAKUTONGOZA NGOJA NIKUPE MAARIFA UMPIME KAMA KWELI ANAKUPENDA KUTOKA ROHONI AU NI ULAGAYI FANYA HIVI HATA MIMI NIMEKUPENDA JAPO SIJAKUONA LAKINI SIJUI KAMA UTAENDELEA KUNIPENDA KAMA UTAJUA HALI YANGU ILIVYO MAANA MIMI NI KILEMA WA MIGUU YOTE KAMA UTASIKIA TENA AKIKUSUMBUA

    ReplyDelete