Thursday, October 21, 2010

NILIKUNYWA SUMU NIKAPATA MUME....

ROSE, najuwa hili jambo ni la kushangaza lakini leo nayaka niliweke wazi kwa watu wajue, na hii pia ni kwa watu ambao hawajaolewa na wanaisi kama hamna mwanaume wa kumuoa.
nilikuwa na mwanaume wangu ambaye nilimpenda sana na kuamini kwamba na yeye alinipenda pia, mpaka siku moja nilipoenda nyumbani kwake na kumfumania na mwanamke mwengine (mwanamke ambaye hata hanifikii mimi kwa lolote lile) baada ya kuona lile tukio roho yangu iliniuma na nikachanganyikiwa sana nikajikuta nimechukuwa sumu ya panya iliyokuwa pale chumbani kwa huyo mwanaume wangu na kuinywa hakuamini kama ningefanya kitu hicho kwa hofu nisije nikafa kufa ndani mwake akanikimbiza hospital na kuniacha hapo bila kunilipia chochote bali kumwambia muhudumu kwamba nilikunywa sumu.
pembeni ya nilipokuwa nimelazwa kuna kaka mmoja alikuja kumuangalia mama yake alikuwa anaumwa, akasikia muhuguzi akiniuliza kwa nini nilikunywa sumu huku nikiwa natapika sana, basi huruma ikamwingia akaja kunihudumia akininunulia maziwa na juisi ya machungwa bila hata kuniuliza jina langu...nilishangaa na kuogopa sana.
nilipotibiwa na kuanza kujisikia vizuri nikamuhadithia yule kaka kila kitu, cha kushangaza akaniambia anataka kunioa, nikashangaa sana kupata mchumba bila kutegemea nikamwambia itabidi tuchukuwe muda kujuana kwanza kabla hatujaoana kwahiyo sasa ninafuraha ya kusema baada ya dhiki faraja mwanaume wangu wa zamani amenipa mume.
Rukia

1 comment:

  1. Hongera Shostito.
    Mungu uwa amempangia kila mwanadamu jambo jema.
    Mie pia nilipewa mimba na Jamaa akaniacha akanipiga na kunipasua usoni kwa kunilazimisha kutoa mimba.Ila sikutoa Maajabu ya Mungu Nikapata Mchumba mimba ikiwa na Miezi 7.na akania ndoa ya kanisani na hivi sasa nakwambia nina Mme na mtoto wa kiume.Hivyo nawashauri wanawake mwenzangu msikate tamaa kwenye swala la maoenzi.Mungu kakuandalia Mme wanko jamani.

    ReplyDelete