jamani malalamiko mengi sana yapo siku hizi haswa kwa hawa waume wenye ndoa wenye tamaa za ajabu, yani kwanza hawatosheki na wake zao, pili hawatosheki na hivyo vimada wanavyopata barabarani, sasa wanachukuwa mpaka wasichana wa kazi sasa wewe mwanaume si unamatatizo tena unapepo la ngono unahitaji kuombewa, haya yamewakuta wengi na wengi yataendelea kuwakuta..
mimi naamini ukishakuwa baba mama anategemea mengi sana kutoka kwako, matumizi ya nyumbani, afya ya wote nyumbani, kutunza familia yako zaidi ubaba wako uonekani kwa upande wa kimwanaume, sasa wewe mwanaume unavyoingilia kazi za mama inakuwaje jamani? mara unaanza kumpangia msichana wa kazi kazi za kufanya, mara unamsema mke wako kuhusu nyumba sijui hiki kimefanyaje mara kile kimefanyaje yani wewe ndio unataka kusimamia mpaka nyumba sasa wewe tutakuitaje? kuwa baba sio baba na mama
ninacho fahamu kama baba ameona kitu ambacho hakijafanyika vizuri humuita mkewe na kumwambia kwa upendo sio unatoa maneno kama rekodi mbovu kumkashifu mkeo na kumtishia maneno kibao ya kuhusu msichana wa kazi kama umalaya wako ni kulala na wasichana wa kazi si ufanye tu sio mpaka utafute sababu.. tum tum umeisoma?
unavyo rudi nyumbani nguo zako huzikuti safi, chakula hukuti kimepikwa, nguo zako zote za ndani anafua nani, kitanda unacholalia anatandika nani na kuhakikisha shuka zako ni safi mda wote, choo unacho tumia na maji ya kuoga anayaweka nani?
waume kwenye Biblia imeandikwa mwanamke mpumbavu ataivunja nyumba yake mwenyewe lakini ninachoamini mimi hamna mwanamke mpumbavu atakaye haribu nyumba yake bila shinikizo la mumewe kwahiyo wanaume jueni mipaka yenu na mjuwe kuheshimu wake zenu kwani kazi wanazofanya ukiachiwa nyumba hamtakaa zijuwe kufanya vizuri kama mwanamke.
nimeisoma hiyo kwa mapana na marefu, yaani wanaume wengine wanadiriki hata kumpeleka shopping msichana wa kazi, walaa sio adiscuss na mkewe,anajiamulia tu na kumchukua msichana wa kazi kumpeleka shopping ya nguvu, ilhali hapo huyo mkewe kumpeleka shopping au hata kumpa hela akfanyie shopping cjui ilikua lini.
ReplyDeletewanaume wanakua hawaheshimu wake zao, wengine tena mbele ya watoto utakuta anapayuka oooh mwanamke gani hujui kupanga nyumba, nyumba chafu hivi na vile, na ntaoa tena mie, kweli maneno ya kumwambia mke wako tena mbele ya watoto?? wababa wanachangia sana pia kuwafanya watoto wakose raha pale wanaona wamama zao wakidharauliwa na baba zao. its a very bad feeling ambayo children carry for the rest of their lives.
wababa wabadilike wawe wanaume kweli si kujivalisha uhusika usiokua wao ili tu kujifurahisha nafsi zao....MEN STOP BEING SELFISH!!
Its me tum tum
Msemavyo wanawake mlioolewa ni sawa. Mimi ni mwanaume. Ila si nyote, wengi wenu mnasahau majukumu yenu na kumkabidhi house girl
ReplyDeletewamama wengine utakuta wanajitahidi lakini wanaume hawaoni. unaamka saa kumi na moja asbuhi, unaandaa vitu vya watoto wako wanaonda shule na wasionda. mume anaamuka saa 1 unamuandali maji ya kuoga na chai lakini, akirudi anaanza kufoka hapa mbona hapaja fanyiwa usafi. hajui na wewe ulienda kazini. na kama msichana wa kazi ndio kabaki nyumba lakini mnapokuwa na mtoto mchanga kabisa, msichana hawezi kuangalia mtoto na mambo mengi. hivyo unakuta wamama tunaumia sana, kulala wamwisho kuaamka wa kwanza
ReplyDelete