Tuesday, August 10, 2010

WANAWAKE WENYE TAMAA JAMANI HAIPENDEZI..

jamani wanawake kwanini wengine hampendi kuridhika na hali mlizokuwa nazo? kama kipato chenu sio cha juu kwanini utake ya juu, kuna dada mmoja hivi ameolewa lakini wifi yake utadhani yeye ndio mwenyenyumba kutwa kwa kakaye anataka kile mara hiki mara vya bei ya juu sawa hatukatai huyo ni kaka yako na uwezo wa kukusaidia anao lakini hufikirii kwamba sasa ana mke ukihudumiwa wewe hivyo huyo mkewe atahudumiwa vipi? haipendezi wewe wifi kuingilia nyumba ya mwanamke mwenzako..
ama shida yako upendeze wewe kaka yako akuoe? mwambie mke wake akupe chumba uone kama utaweza kumtimizia kaka yako, kwanza unajuwa hizo hela anatoa wapi ama kimbelembele tu kimekujaa haya sasa kama anakopa kwa kukupendezeshea wewe na akishindwa kulipa akiingia matatizoni familia yake utaitunza wewe? (nadhani mawifi wa tabia hii mtakuwa mmenipata haswa)
zamo yako ilishaisha alipoamua kuoa, muache ale ndoa yake kwa amani na mkewe, katafute wako akutimizie na hivi wenye pesa mjini siku hizi wa kumwaga, achana na kaka yako atunze familia yake.

1 comment:

  1. jamani dada rose mimi ni mpenzi sana wa kutembelea hii blogger nikotofauti na mada kidogo nilikuwa naomba hata kama niwewe mwenyewe utakuwa unafahamu website ya katuni za kiswahili kwani huwa nazipenda sana zinaniburudisha sana nazielewa website chache tu natumaini ziko nyingi ambazo zizielewi naombeni na wadau wengine wanaofahamu wanijuze pls mbarikiwe sana

    ReplyDelete