Monday, August 9, 2010

MBONA SIBEBI MIMBA?

Rosemary Mizizi, nina mwaka sasa najitahisi kweli kupata mimba lakini kila ninavyojitahidi sipati mafanikio,mpaka nikaenda kusafishwa nikidhani kuwa labda mirija yangu itakuwa imeziba lakini baada ya kupitia maumivu yote yale ya kusafishwa bado sijabeba mimba na kwenye ukoo wetu hamna tasa wote wamezaa Rose hebu nisaidieni nifanyaje?

Teddy

JIBU

pole sana kwa hayo yanayokupata, nakushauri hivi ukiona mkao wa kawaida wa kitanda haukupi mtoto basi badilisha geuza kitanda kama kinageukia juu kigeuze chini,kama bado hujapata basi geuza tena upande mwengine, na kama bado weka hata godoro chini na mtunge mimba lakini kabla ya kuanza kutunga mimba muombe Mungu kwanza abariki lile tendo ambalo ni la halali kwani zawadi kuu ya Mungu baada ya ndoa ni watoto.na kumbuka wakati mwengine mwanaume mbegu zake haziendi mbali basi jaribu kuweka mto chini ya mapaja yako ili kiuno kiinuke na mbegu ziweze kufika mbali.

1 comment:

  1. pia mweleze huyo dada akacheck hospital kama anafibres ni uvimbe unawakuta wanawake wengi ila uko tz huwa hawaangalii madtari huwa inasababisha kutoshika mimba. kama yuko vizuri kifedha mweleze asafiri nje ya nchi kimatibabu watamweleze kama anamatatizo yoyote yale hapo tz wanaweza wakamfanyia operation za bila sababu wakamwalibu tu yalimpata ndugu yangu.mdau wa texas

    ReplyDelete