jamani nataka leo tuliongelee hili jambo, unajuwa wakati mama anapokuwa amejifungua wataalam husema ya kwamba kizazi chake huwa wazi tayari kwa kudaka mbegu pindi itakapoingia, sasa basi inakuwaje pale pindi mnahamu ya kupeana penzi na baba kumwaga nje hataki? inafaa kuvaa condom? na najuwa wanawake wengi watakubaliana na mimi kwamba hawajali wapenzi wao wakivaa condom lakini kwanini hii huwa ngumu sana kwa wanaume, na maranyingi husema mke wangu mwenyewe nitamvaliaje condom (haya ni maneno niliyoyapata baada ya kuhoji wame za watu)
wewe kama mume swala la kuvaa condom na kumpa penzi mmkeo unalichukuliaje na wewe kama mke wakati unpohitaji mwenzi wako avae condom kama kizuizi cha mimba na akakataa unahisi je ama unamchukuliaje mwenzi wako kwa hilo jambo?
No comments:
Post a Comment