mimi ni msichana, nimeolewa na ninawatoto mume wangu na mimi tulikuwa tunapendana sana lakini kwa muda sijui kitu gani kilitokea tukawa tu hatuelewani, mara kwa mara tunagombana vitu visivyo hata na msingi ikafikia kipindi mume wangu anatishia kutaka kuondoka nyumbani, na kipindi hata hana hamu ya kuja nyumbani akirudi yeye kutwa anakaa kwenye pombe akirudi ni kulala tu hata kunigusa hataki kabisa kwahiyo yale mapenzi ya mwanaume nikawa siyapati kabisa.
wanangu nao hawapati mapenzi ya baba yao maana mwanaume kutwa anaondoka asubuhi na kurudi saa tano za usiku wakiwa wamelala na hata kama akiwakuta macho hawezi kukaa nao mda mrefu maana anakuwa amelewa kwahiyo huenda kulala moja kwa moja.
muda ukafika nikawa nahitaji mapenzi ya mwanaume, nahitaji nishikwe, kubembelezwa, na kukumbatiwa japo hata kwa muda mchache, siku moja nikaja kukutana na kaka mmoja yule kaka anakila kitu ninachopenda kwa mwanaume,alinitamkia kunitaka kimapenzi nami sikusita kumwambia nina mume na watoto na kwavile nilikuwa nahitaji pendo kutoka upande wa kiume nikampa kaka nafasi.
yule mwanaume akaanza kunionyesha mapenzi ya ajabu ambayo hata kwa mume wangu sijayapata, yani nisipokuwa naye siachi kumuwaza maana amenichanganya kabisa na nahisi thumuni lake ni kunifanya nimsahau mume wangu nimuone kama kaka yangu maana hata nikirudi nyumbani sina hamu kabisa na mume wangu yani na hivi yeye hanigusi basi mimi furaha kwangu maana kutwa yeye akija analala kama gogo.
sasa hivi imefika siwezi kumaliza siku bila kumuona huyu kaka nahisi siku yangu haijakamilika na kama sijamuona basi ataongea nami kwenye simu hata mara tano kwa siku, huyo mume wangu mpaka namuonea huruma maana sijisikii tena kitu juu yake jamani, mpaka nahisi nimelogwa ama ni kwavile huyu kaka ananipa mapenzi ambayo mume wangu hanipi?
Ndivyo maisha yalivyo. Muosha huoshwa. Wakati unaendelea na huyo kaka;jua kuwa na yeye anaendelea mahali, kwa hiyo bilabila.
ReplyDeletePamoja na hayo bado hiyo si suruhu ya matatizo yako, furahisha nafsi yako lakini kwa mume utarudi tu.
Unafurahia na huyo kaka kwa kuwa mnaishi mbalimbali, lakini ingekuwa mnaishi naye kama mumeo (yaani huyo kaka akiwa mumeo) basi ungemtamani huyo mume wako (mume halali wa sasa akiwa kidumu cha nje) na kumwona mzuri.
Matatizo yako kwako.
mpende akupendaye ndugu yangu maisha yenyewe mafupi nahuyo anayesema matatizo yapo kwako yeye kaolewa anajuwa raha zake na shida zake?
ReplyDeletekama huyo kaka anakupenda basi nawe usisite kumpenda maisha yenyewe haya mafupi hilo gogo liache lilale wewe shida zako si unatimiziwa?raha ya kupenda upendwe
hii mada ningependa sana niichangie hivi,mimi kama baba niliye kwenye ndoa huu ni mwaka wa 17sasa nataka kumueleza huyo dada hivi, uvumilivu ni kitu cha muhimu sana, kwani jambo kama hilo ni la kawaida kwenye ndoa kuna wakati mwanaume anakuwa tu hana hamu na mkewe (kumbuka sio mara zote kwasababu anatoka nje hapana)hii ni inatokea tu na wakati mwengine pia mwanamke anakuwa hana hamu kabisa ya mapenzi lakini sio anatoka nje, na hata kama huyo mumewe anatoka nje hilo ni jambo la muda tu,wanaume wengi hupitia hivyo lakini muda fulani hurudi na kutulia na wake zao,cha muhimu ni kwamba wewe umeolewa na mwanaume lazima arudi hapo kwako kulala na sio kwambva muda wote hata kushika kunawakati anakuwa na hamu sana ya mke wake hapo ndipo umpokee penzi lake,hilo lisikukwaze kabisa kama umeamua kuwa na huyo kaka endelea naye lakini asikufanye umsahau mumeo kabisa kumbuka uliapa kuwa naye kwenye shida na raha.
ReplyDeletedada kua makini ktk ndoa kutafuta suluhisho ni jambo jema kuliko kukaa kimya kwani kote huko c kujenga ni kubomoa kwani ipo siku mtakuja umbuka,matatizo yapo ila communication kwenu ni tatizo,vunjeni ukimwya!na wote kua na nafsi yenye kumwogopa mungu istoshe magonjwa....utafurahia sasa na kutake easy ila itawacost.kaa chini jaribu kujishusha kwa mumeo mjadiliane that how marrige iz.
ReplyDeleteni sawa dada hongera sana tena jirushe kwa raha zako maan hawa wanaume wanachosha sana, mwenyewe nimeolewa ni muda sana mume wangu hatufanyi mapenzi huwezi amini kuna wakati najisikia hamu sana hata umvuteje hataki tena ananiambia wazi kuwa nenda kokote, sasa nina miaka karibu miwili jamani nimemvumila vya kutosha na kipindi chote hicho nimeshamfumania na amezaa nje tayari ila nasamehe coz mi ni mkristo hasa kutwa ana wanawake. sasa kwa mtindo huu mtu utaacha tu kutoka nje ya ndoa jamani? maan binadamu unaekula protein kuna kipindi joto la mwili linakupanda na wewe unahitaji mtu akutimizie sasa utafanyaje?kwa kweli hawa wanaume wanatulazimisha kutenda jambao ambalo mtu hukupanga kabisaaaa.
ReplyDeletekwahiyo shost we jirushe tu kwa raha zako, ila be careful huyo mmeo asije akakukuta maan atakuua.
Dada wewe umepata njia mbadala ya kupata furaha na kufarijika moyoni. Hivi ulikaa ukawafikiria wanao?????? Wao wanafarijika kiaina gani???? Watoto ni baba na mama, ni dhahir kuwa wanao hawawezi kukaa na huyo mwanamume wakaongea nae kama baba na kutoa matatizo yao kwake. Wao umewafikiria vipi???? Je uko tayari mumeo akupe talaka uwache wanao wakalelewe na mama wa kambo??? Kwani kama hayuko tena moyoni itafika siku utadai talaka ukastarehe kikamilifu na huyo mwanamme. wana jeeeeeee? Fikiria zaidi na muanze kuongea, matatizo mume na mke madhal mnaishi pamoja ni GIVEN, huwezi kuepuka hayo. Huyo saint wako ukija ishi nae pia atakuwa kama huyo mumeo mwishoe. Kaeni kitako muyaongee muyarekebishe mulee watoto wenu kwa amani. Don't be selfish.
ReplyDeleteWanasema ukizini nawe utaziniwa, na wengine wanasema unapofanya mapenzi nje ya ndoa, ujue nawe utafanyiwa. Lakini kwanini mpaka ifikie huko, kwanini watu wasike wakaongea.
ReplyDeleteMimi nimegundua kuwa tatizo kubwa ni mawasiliano, na mawasiliano haya sio haya ya kuongea kikawaida, bali yale yakuelezena kinagaubaga, nini unapenda mwenzako akufanyie na afanye nini na mahala gani ili ujisikie.
Kwa wanaume mke mnzuri ni yule anayejua tendo la tendo, na kwa mwanamke mume mzuri ni yule anayemjali kwa kumsikiliza shida zake, wakati mwingine sio lazima kwa tendo la ndoa.
Ukiona mke anahitaji tendo la ndoa na analikosa kwa mumewe, kuna walakini, hasa kwa huyo mume, labda amepata vishawishi au anafanya kazi nzito zinazoathiri ashiki yake au ndio havutiwi kwasababu na wewe mke hujiweki kumvutia.
Yote hayo nimeyataja lakini ukichunguza ni udhaifu wa kibinadamu wa kutokuwasiliana na kuelezana ni nini kifanyike ili pendo lidumu. Pendo ni sawa ni vitu vingine vinahitaji kujifunza na kufunzana, unaweza ukamapata ajuaye au asiyejua, lakini akifundishwa au mkifunzana mnaweza mkamzidi hata huyo alieyejua mapema.
Dawa sio kuruka ukuta, hiyo ni hatari kubwa sana, sijui mwenzako akigundua ataumia kiasi gani, kwa mafano kama hana tabia hiyo ya kwenda nje ya ndoa, dawa sio kumuacha mumeo kwasababu huenda huyo unayemfuata kwasababu ya hilo tendo huenda ana kasoro nyingine amabazo ukigundua unaweza ukajuta, kwasababu binadamu hatujakamilika kwa kila kitu.
Kaeni muongee, mjadili na huenda mkarejesha pendo lenu kama awali.
Pole sana dada kwanza elewa kabla ya wewe kupata huyoo kijana tayari mmeo alishapata mwanamke siku nyingi sana na ndoa mana hana mda na familia yake.Nakwambia hivyo mana mie pia imenitokea kama yako.ila mie sina mwanaume mwingine nimeamua kukaa na kulea watoto.
ReplyDeleteWaume zetu ndo wanafanya na sie tunatafuta mapozeo kwa vijitabia vyao.
Ila wangu kuwa makini na kamchezo hako unakocheza usinogewe sana.
Hii ndio akili ya mwanamke, kwenye maelezo unasema watoto wanakosa mapenzi ya baba. sasa huyu jamaa umrtabulisha kwa watotoawape mapenzi?
ReplyDeleteHakuna uchawi wala nini, wewe una pepo la ngono tu. halafu mbona wanawake wanaonyesha kama wao hawafurahii mapenzi ila wanatusadia sisi wanaume?
Naomba Mungu ushikwe/ufumaniwe au upate ugonjwa ili ujue mshahara wa dhambi ni mauti.
Nafikiri mwanamke kama wewe una pepo wa ngono tu, maana baada ya hapo pia utahamia kwingine, halafu mwisho wa siku utahamia kabisa barabarani kuuza kwa bei nafuu. Jitahidi mamaa kama wenzako walivyotangulia kukushauri kwa raha zao au c o ?
ReplyDeletepole sana dada,njia unayotumia kusuluhisha tatizo sio....kama kuna kurogwa basi mchawi ni wewe mwenyewe!kaa chini ongea na mumueo lakini kwanza acha uyafanyayo kwa dhati mwombe Mungu akusamehe then angalia jinsi ya kumaliza tatizo hilo!
ReplyDelete