SWALI: ndoa ni nini, ni kufanya mapenzi tu?
JIBU:
kuna mtu ameuliza hilo swali hapo juu japo hakutaja jina lake mimi nataka nimjibu ninavyofahamu na wewe umuelezee jinsi ujuavyo..
kibiblia ndoa ni pale wawili wanapokutana kimwili katika kufanya mapenzi, maana kile kitendo unakuwa mmepeana kila kitu chenu kutumia hisia na ndio maana hata ukilala na mwanaume zaidi ya mmoja basi hao wote umefunga nao ndoa na mnapeana vile mlivyokuwa nayo kama mabaya na mazuri (wewe unampa yule na yeye anakupa wewe)ndoa ya aina hii wengi wameifunga maana haitaji sherehe kujuwa umefunga na wengi hufunga sio na mtu mmoja bali watu tofauti hiki ni kitu cha kawaida kwa maisha ya sasa.
kijamii ndoa ni pale wawili wanapoamua kuacha wazazi wao na kuungana kuwa kitu kimoja pale kanisani, halafu ya kimwili hufwata baada ya hapo na hapo ndipo kila mtu anajuwa fulani ni mme ama mke wa fulani wanapoapa kuwa pamoja kwenye shida na raha, hata kama lipi likitokea kutokuachana mpaka mwisho wao na watoto wao. na ndoa hii wengi huitaka kwa garama yeyote ile ilimradi tu nawao waonekane wameolewa lakini sio kwamba ni kwa mapenzi ya kweli.
Swali kama hilo wengine wanajiuliza wakati wameshaoana, na kukutana na vikwazo anuia.
ReplyDelete'Hivi kweli ndoa ndio hivi, mbona wale wapo vile, kwanini mimi imekuwa hivi, mbona...nk'
Ingekuwa vyema watu wakitka kuoa au kuolewa wangepitia semina au hata shule ili waelewe vyema nini maana ya ndoa, sio kuilewa kitafsiri, bali kimatendo, kwani unaweza ukaelewa kitu kitafsiri, lakini kimatendo ukajikanyaga.
Wengine wanalichukulia juu juu tu wanasema mtajifunza mbele kwa mble, na matokeo yake mnayaona, nyumba zinakuwa hazina amani, hazijui nini maana ya upendo, na matokea yake wanzaa kizazi kisicho na upendo na mwisho wa siku taifa linakuwa lisilo na upendo.