Thursday, July 15, 2010

HESHIMA NDANI YA NYUMBA....



nyumba katika maisha ya wanandoa sio hilo pango ambalo watu huishi ndani, nyumba ni baba, mama na watoto pamoja na hilo pango linalowastili na ndio maana ikaandikwa ndoa iheshimiwe na watu wote iwe baba, mama ama watoto au hata watu wote wanaokaa pamoja nanyi kwenye nyumba yenu...
heshima ni kitu cha bure hakiuzwi jamani sasa inakuwaje nyumba hazina heshima, mama akisafiri baba analala na msichana wa kazi baba akisafiri mama anaingiza mwanaume ndani hivi ni vitu ambavyo kila siku tunavisikia..
ama inakuwaje baba kila kukicha unarudi usiku wa manane nyumbani kwako yani panakuwa kama gesti wewe unaenda lala tu lakini kutwa mguu na njia mkeo akikuuliza unasema eti baba hana muda maalum wa kurudi nyumbani inahusu jamani (shosti umenipata) yeye kila mara achelewe ukimwambia inakuwa ugomvi mpaka majirani wananchungulia kwenye madirisha mnachekwa nyie haipendezi jamani..
watoto wanataka wamuone baba yao ama mama yao asubuhi na jioni wanategemea baba ama mama uwaulize wameshindaje wakueleze siku yao ilivyokuwa sasa wewe uwaone tu hasubui utakuwa baba au baba jina nawe utakuwa mama au mama jina haipendezi jamani..
watu starehe wanazifanya za aina zote lakini pia huweka familia zao mwanzo, sasa nyie mking'ang'ania starehe mwanzo hata hao watoto wenu hawatakuwa na mapenzi ya dhati kwako, mapenzi yanajengwa hayaji tu kama ndoto (shaurilo)

0 comments:

Post a Comment