sisi wanawake mara nyengine jamani.... kuna dada mmoja ameolewa ana miezi mitatu tu kwenye ndoa, mumewe gafla akapata safari ya mbali kumbe huyu dada yeye alikuwa na kidumu pembeni ambacho inasemekana alikuwa naye kabla hata ya ndoa, mumewe aliposafiri yeye akaona huo ndio muda wa kutanua na kidumu chake....
juzi wakapanga waende gesti kulala, wamefika vizuri wakaagiza chakula na vinywaji chumbani wakala na kunywa kwa mapenzi tele, shughuli ikaanza jamaa alipofika kileleni akalala kwa sababu ya uchovu maana alikuwa hajapata siku nyingi maana tenki(mume) wa yule mama alikuwa anambana sana mkewe kutoka..
basi yule dada naye akapumzika pembeni ya kidumu chake, mara lisaa likapita dada akaamka akawa anampapasa kidumu ili apewe mzunguko mwengine ndio balaa ilipoanza, amsha, amsha,amsha na wewe wapi jamaa haamki lisaa lizima haamki mama sindio akachanganyikiwa na kuanza kupiga kelele kuomba msaada....
watu wakaja, polisi wakaitwa sasa dada akapata kiwewe alipopelekwa polisi analia jamani nisaidieni niacheni niondoke mume wangu atakuja kuniua ndoa yangu bado changa jamani...
likamkuta huyo bishosti analo sasa hivi analilia polisi....
Jamani, jamani. Hebu naomba tuelewane, ukisha amua kuwa kwenye ndoa, maana yake umekubali kuwa na huyo tu awe mwenza wako, mambo ya kujichanganya nje ya ndoa ni mabaya, kama unaona huridhiki na ndoa yako, basi mueleze mwenzio mtafute jinsi ya kurekebisha mambo, kama haiwezekani kabisa basi omba talaka.
ReplyDeleteKutembea nje ya ndoa ni dhambi kubwa sana na mbaya, Mungu hapendi. Kwa wale wakristo wanajua imeandikwa kuwa, ndoa na iheshimiwe na watu wote na malazi yawe safi, mtu wa kwanza kuheshimu ndoa ni wanandoa wenyewe. Ukishaenda kinyume na agazo hili la Mungu, ujue atakuadhibu tu. Mojawapo ya adhabu ni kama hayo yaliyo mkuta huyo dada yetu. Hata kama polisi watamuachia, sina uhakika kama ndoa yake itakuwepo tena. Naomba tena waliopo kwenye ndoa, tuache kujichanganya, madhara yake ni makubwa! Haya ndiyo niliyo nayo kwa leo! Obazega!
jamani dadarose mimi nikonje ya mada kidogo naomba unisaidie namna ya kupata wimbo wa jojina wa mamaa niko nje kidogo ya nchi sasa nataka kujikumbusha huo wimbo wa jojina pls ikewezeka uniwekee ktk hii blog yako au unionyeshe namna ya kupata huu wimbo maana nimejaribu youtube sijafanikiwa hata sikumbuki nina aliimba huu wimbotafadhali mpedwa unisaidie ubarikiwe
ReplyDeleteHuo nao unafiki. Anajifanya anampenda mumewe wakati amesariti. Ndio ndoa za kisasa, watu wanatafuta kuvaa pete ili kuondoa mkosi, lakini ndoa/mapenzi hakuna.
ReplyDeleteYawezekana mume alishitukia mapema akaweka mtego wake.
hiilo kihseria sio kosa saana kwani watapima na kuona nini kimumuua jamaa. inawezekana alikuwa na ugonjwa kibao au presha. mtu anakuwa na presha harafu mdada anamtwanga romance ya nguvu jamaa anapitiliza. si unajua wakiona unateseka ndo wanataka waongeze chumvi??
ReplyDeletekwa hiyo mdada hajasababisha kifu wala kuua bila kukusudia, atakuwa huru ila soo ni ndoa yake ikizingatiwa kafanya mapenzi na marehemu!!!
mambo ya nje ya ndoa yanapendeza na kuwa matamu kama hujakamatwa au sio??