Friday, June 4, 2010

WIVU........

wivu ni kitu kibaya sana kama wivu wako wewe utakuwa wakutokupenda maendeleo, na wivu ni mzuri sana kama wivu wako ni wakupenda maendeleo, kwa kupenda namaanisha nini? kwa mfano umeona jambo ambalo mtu fulani kafanya labda kajenga nyumba nzuri ni vizuri kumuonea wivu ili na wewe uzidi kujitahidi upate nyumba japo hata kama sio nzuri zaidi ya kwake..
lakini wengi huwa na wivu mbaya, watu mpaka wanagombana, wengine wanawivu wa kijinga mpaka wanalogana, eti kisa mtu fulani kwao kila mara wala kuku na wewe wala maharage..
mwanamke unawivu kisa mwanaume wako wa zamani kakuacha kampata mwengine, unawivu mpaka unaenda kuwafanyia vurugu (inahusu jamani) wewe kama chako hamna si hamna tu, huyo mwanaume si kakuacha kisa kakuona haufai kuwa wake ungekuwa unafaa siangekuoa akuweke ndani????? jamani tunajua kuachwa kunauma lakini utafanyaje hata ukiwafanyia vurugu unadhani utaolewa wewe?
ama mwanaume kisa umeachwa ndio unaongea mambo machafu kuhusu mwanamke wako wa zamani, oohh kwanza sura yake mbaya ina makovu, mara mwanamke mwenyewe ananuka, mara mshamba, mara kuvaa hajui, ohhh mara useme mtu mwenyewe kitandani hana kitu, mara huyo mwanamke alinitongoza mwenyewe sasa jamani hayo yote hukuyaona mlivyokuwa wote na isitoshe huyo mwanamke unayemtukana mkikutana chobingo unaomba kiuno(hunahaya unalo ilo)...
mara kisa mdada wa watu katoka familia bora wewe kwa wivu wako mmbaya unaanza kumsema, yule nae anaringa, anajifanya tajiri, mara yupo amayai hata kazi kufanya hawezi sasa wewe ndugu yangu kama umezaliwa kijijini si wewe ama kama hujazaliwa familia ya kitahiri si wewe kumsema msichana wa watu inahusu nini???????
wivu jamani looooo, kama huwezi kuwa nacho huwezi tu hata kama ukitukana, ukimsema mwenzio chake chake tu kama chakula utabaki kula ukoko tu wali ala mwenyewe tafuta chako...

1 comment:

  1. dada yangu hili ni tatizo kuna dada mmoja anampenda kaka asiyempenda licha ya kujipendekeza kila mara hatakiwi tena hilo li dada lina mizwia na limepigwa pasi, kwa maana nyingine halina shepu.jamani ache kama hampendwi

    ReplyDelete