binadamu yeyote uwe umeoa ama hujaoa, umeolewa ama hujaolewa, mfupi ama mrefu, mweupe ana mweusi ukivaa vizuri lazima utapendeza, kwani uzuri wa kwanza hutakana na muonekano wako wa nje yaani mavazi yako na ufahamu ya kwamba kupendeza sio mpaka uwe umevaa nguo za bei kubwa..
jamani huku barabarani kweli kunavituko nimeona wakaka na wadada wazuri lakini cha kushangaza utakuta wamezaa nguo zilizopauka utakuta mtu amevaa suruali kali kweli lakini ukimuangalia shati ama top aliyovaa jamani nikichekesho yani vimepauka mpaka aibu utakuta kama nguo rangi nyeusi inakuwa imepauka mpaka inabadilika rangi kuwa nyeupe jamani haipendezi hata kidogo..
na sio kwa mavazi ya nje tu utakuta hata nguo za ndani yaani zimepauka mpaka aibu halafu mtu bila aibu anavaa nguo fupi ama suruali ndio yakuvaliwa mlegezo ukikaa chini mpaka aibu ..
ama kwa wale wanaofua nguo za ndani na kuzianika nje, kama unakaa nyumba ya peke yako inageti lako sawa unajua hata kama ukifua nguo zako za ndani aibu unaijuwa mwenyewe kama zimepauka sasa kwa wale wenzangu na mie tunaokaa nyumba za kupanga zisizokuwa na mageti halafu kamba za nguo unatumia na wapangaji wenzako halafu unafua nguo zako za ndani na zimepauka unaanika nje jamani sio aibu hii mpaka majirani siwatakucheka??haipendezi kabisa...
kama tunafua nguo zetu za ndani nakuanika nje basi tuhakikishe ni nyeupe ama zile ambazo hazijapauka rangi, na kama unanguo za ndani zilizo pauka sio vibaya ukijitahidi kununua mpya jamani, hata kama pesa hauna ya kununua nyingi tujaribu kununua hata moja moja itasaidia..
hayo ni mawazo yangu tu..
No comments:
Post a Comment