Monday, June 28, 2010

TUMBO KUHARIBIKA WAKATI WA UJAUZITO......






hakuna baraka kubwa duniani kama baraka ya kupata watoto, na hakuna mtu muhimu kama mama anayebeba mtoto kwa miezi tisa raha na maumivu yote huyapata mama, na hata kama mama huyu huwa mwenye umbo zuri sana kabla ya ujauzito wengi uzuri wa umbo (haswa) tumbo hubadilika baada ya kuwa mjamzito.....
wanaume mara nyengine huwasema sana wake zao kwa kuwa na matumbo kama haya, ni vizuri wanaume kuelewa kwamba wanawake hutofautiana, na kama mkeo/msichana wako amejifungua kwa operation huwa mara nyingi hawafungi tumbo.....
na wakati mwengine hata kama hujajifungua kwa operation inaweza kutokea ukafunga tumbo halafu bado likakataa kurudi(hiyo nimeona kwa wengi tu)........
cha muhimu wame zetu waelewe ya kwamba hatakama tumbo likibadilika lilibadilika kwa wema na baraka ya kuleta viumbe duniani, watoto damu zao kuliko kuwasema na kukasirika wake zenu kuwa na matumbo mabaya hebu washukuru hawa wake kwa kuwaletea watoto, ambao kila siku mnatembea kwa sifa kwa kuitwa baba fulani.......

No comments:

Post a Comment