Thursday, June 3, 2010

TATOO ZA WANAWAKE.......

tatoo ni kitu ambacho unahitaji ujasiri sana kukiweka katika mwili, wanawake wengi wamekuwa wakiweka tatoo kwa maana tofauti wengine kwasababu rafiki zao wameweka kwahiyo ili uonekani na wewe upo inabidi uweke, wengine wameweka tu kwasababu wenza wao hupenda tatoo ndio maana wakaamua kuweka..



kunarafiki yangu yeye amechora uwa linalotoka kwenye kiuno upande wa mbele kuelekea kwa bibi anasema shanga kuvaa hajui, kwahiyo kuwavutia wapenzi wake ndio ameamua kuchora hiyo tatoo kubwa ya ua kuzunguka kiuno kama shanga, anasema mpenzi wake akiona tu yani hata kama chakula chausiku alikuwa hana hamu basi njaa inaanza gafla..



wengine hochora jina la wapenzi wao kwenye miili yao, lakini sasa kama huyo mpenzi wako mkiachana inakuwaje? ama ndio mapenzi ya kizungu haya jamani,... haya bwana hapo mimi ndipo paliponishinda...




kwa uzuri ama ubaya tatoo zimekuwa zikiwapendeza watu wengi sana haswa wadada maalum sehemu za kiuno..

1 comment:

  1. Karibu dada kwenye blogu. Nimeipenda blogu yako. Nadhani itakuwa na vipya...karibu sana.

    ReplyDelete