Thursday, June 3, 2010

SABUNI YA KUOSHA KWA BIBI..

kuna sehemu nilienda siku moja nikakuta panauzwa sabuni ya kuosha kwa bibi sabuni hiyo ni ya majimaji japo ni nzito sana kwa kuitazama tu kwenye chupa yake jamani inapendeza lakini bado najiuliza hizi sabuni za kuosha kwa bibi hazina madhara? je kunamtu ambaye ameshawahi kutumia akatufaamisha? kwasababu ninajuwa na nimesikia sabuni nzuri ya kuosha kwa bibi ni maji ya uvuguvugu pamoja na mkono wako, kwani watu wengine pia wanasema wamejaribu kutumia hizo sabuni wakawashwa sana lakini cha kushangaza kuna wengine wengi tu wanatumia kujioshea na wanazipenda sana...


kwa wewe mwanamke mwenzangu sabuni yako ni nini?

1 comment:

  1. Ndio, zipo sabuni maalumu za kuoshea kwa bibi, sababu sabuni za kuoshea kwa bibi huwa haina marashi aina yoyote, na inakubalika huko kwa bibi, lakini mie nipo nje ya tanzania, na hununua pharmacy, na imekua imeandikwa kwamba ni ya kwa bibi, inakuwa ghali kidogo, na ni ya maji maji tuu, hata kuna wet tissues za kwa bibi, ambazo zinapatikana pharmacy vile vile, ni nzuri, zinakunusuru na harufu ya ukeni, na magonjwa fungus na kadhalika.

    ReplyDelete