Wednesday, June 30, 2010

SARATANI YA KIZAZI.......



zaidi ya kupeana mawazo ya mahusiano pia tunahitaji kufaamishana kuhusu magonjwa ambayo ni hatari yakifika katika nyumba zetu, kwani siku hizi magonjwa yamezidi jamani...
kuna kipindi nilisikia Dr mmoja akizungumzia saratani ya kizazi katika redio na ikanivutia na kunisikitisha ikabidi niisome kwa undani zaidi hii saratani ya kizazi na sasa nataka kukupa na wewe taarifa hii ya saratani...
saratani ya kizazi ni kutokukuwa kikamilifu kwa chembechembe hai zinazotengeneza kizazi....
SARATANI YA KIZAZI HUSABABISHWA NA NINI?
kama mwanaume ana mpenzi zaidi ya mmoja(ambaye ana chembechembe za saratani) na hukutana naye bila kuvaa condom, baada ya hapo aende kukutana tena kimwili na mwanamke wake tena bila condom hapo huchukuwa zile virus kutoka kwa mwanamke wa nje kupeleka kwa mwanamke wake wa ndani................
kwa mwanamke ambaye ameanza kufanya mapenzi katika umri mdogo ambao mara nyingi ni chini ya miaka kumi na nane (18)..............
ama kwa mwanamke mwenye wapenzi wengi pia huwa katika risk ya kupata saratani ya kizazi......
na umasikini pia husababisha saratani ya kizazi haswa pale wanawake wanaotumia miili yao kufanya biashara ili kupata pesa za kujikimu.........
wanawake wanaovuta sigara pia huwa na risk kubwa sana ya kupata saratani ya kizazi............
mwanamke kutokula mboga za majani na matunda husababisha risk ya kupata saratani ya kizazi....
DALILI ZA SARATANI YA KIZAZI......
kutokwa na damu zaidi ya kawaida wakati wa hedhi na kukaa kwa mda mrefu
kutokwa na damu baada ya kukutana kimwili
kutokwa na majimaji mara nyingi sehemu ya mwanamke na yenye kutoa harufu mbaya
na kuumwa sana tumbo chini ya kitovu
CHA MUHIMU KUFANYA.........
kama hatuwezi kuwa waaminifu tuhakikishe tunatumia condom na tuhakikishe kama wanawake tuwe na mpangilio wa kwenda hospital na kucheki afya zetu na zaidi ya hapo kama wazazi tuwe wazi kwa wototo zetu kuhusu hili gonjwa...

2 comments:

  1. kweli hii ni mbaya


    Theresia

    ReplyDelete
  2. pia check up inaitwa smear test every two yrs kwa kila mwanamke,kwa huku nchi za wenzetu wanahamasisha sana hiyo check up ndio maana rate ya wanaokufa na huo ugonjwa ni chache.

    ReplyDelete