jamani kuna dada mmoja amenitumia mail anaswali kuhusu hizi cream ambazo tunazipaka, maana siku hizi wanawake na wanaume wote wanashiriki katika upakaji wa cream..
anasema yeye alivyokuwa bongo alikuwa anatumia cream ambayo hajanipa jina lake na ilikuwa inampenda sana na kumfanya ngozi yake kuwa nyeupe na nyororo, lakini akapata safari ya kuhamia ulaya sasa anasema amejaribu cream za huko ulaya na hazijampenda kabisa mpaka zinamuotesha mba usoni na badala ngozi yake kuwa nzuri imekuwa ya kutokuvutia...
anaomba ushauri afanyaje kuhusu hili swala maana badala ya ngozi yake kuwa nzuri kwa cream original za ulaya cha kushangaza huko kwenye cream nzuri ndio zimemkataa afanyaje?
mimi ningemwambia kama anaweza kwenda hospital kwa doctor wa ngozi apate ushauri kuhusu ngozi yake naamini craem ya ngozi yake haiwezi kukosekana hapo.. ama kama atashindwa kilichobaki ni kuagiza cream ambayo anaitumia hapa bongo wamtumie huko ulaya..
wewe msomaji je unamwambiaje?
No comments:
Post a Comment