Friday, May 28, 2010

RAHA YA MKEKA.........

mkeka ni kitu muhimu sana kuwepo nyumbani kwetu, japo wengi hudhani ni watu wa pwani tu hupendelea kutumia mkeka, ama labda kwavile watu wengi hawatambui matumizi ya huo mkeka..

raha ya mkeka ukaliwe bibi, jioni ile siku ambayo wote mpo nyumbani sio mbaya watoto wakiwa nje wanacheza utandike mkeka ukumbini ama hata barazani kukiwa hamna jua uandae na kahawa na haluwa, tende ama kwa sie wapenzi wa juice uiweke pale ikiwa kwenye jagi la mvuto, mkaribishe mpenzi wako mkae wawili ukipenda umlalie ama akulalie kwenye miguu mkitafakari maisha yenu pamoja na ya watoto wenu..

kuna wakati pia hujisikii kukaa mezani kula na watu wengine ama labda mpo wawili tu nyumbani kwenu basi sio mbaya siku moja moja ukatandika mkeka wako chumbani ukaweka chakula kidogo mkaamua kuhamishia meza chumbani kwani wakati mwengine baba hupenda mkewe akimlisha na haipendezi watoto wakaona baba anapokuwa analishwa na mama..

kwa wale ambao wanachoka mara nyengine kulalia kitanda, kwanini usijaribu kutandika mkeka na ukashusha godoro lako ukalala chini, mgongo ukapata kunyooka, huku pembeni ukiwa umekumbatia kilicho chako... hehe

jamani sababu za kuwa na mkeka nyumbani ni nyingi sana hizo ni chache tu, na ndio maana mama zetu kati ya zawadi nyingi wanazotupa basi mkeka lazima huwa moja wapo kwani wanadhamini sana matokeo yake.

No comments:

Post a Comment