Monday, May 31, 2010

KUWASHWA BAADA YA KUNYOA....

jamani wenzangu kuna dada mmoja amenitumia msg through blog hii anajambo ambalo linamtatiza kwa muda sasa baada ya kunyoa sehemu zake nyeti baada ya muda huwa anawashwa, anaomba ushauri wenu zaidi juu ya hilo....

tatizo la kuwashwa baada ya kunyoa kwa ninavyo fahamu mimi maranyingi husababishwa na kitu unachotumia kunyolea, kwani wengi hutumia wembe, wembe wa aina yeyote ile huwasha baada ya kunyoa na mara nyengine mpaka ikakutoa vipele vidogo vyenye maji na huuma sana vikitumbuka..

na wakati wengine huwashwa kwasababu ya dawa za kunyolea, siku hizi dawa za kunyolea zimekuwa nyingi sana, sasa dawa hizi unaweza ukatumia na kukusababishia muwasho baada ya kunyoa, kwani zinaweza zikawa hazipatani na ngozi yako..

hizo ndio sababu mbili kuu ninazo zifahamu, kwa wengine wote wenye sababu nyengine tafadhali tumsaidie huyu dada ajue jinsi ya kutatua hilo jambo alilokuwa nalo...

1 comment: