▼
Wednesday, May 12, 2010
NDOA ZETU......
jamani hivi tunajua maana ya hizi pete za ndoa ama tunazivaa tu kama urembo..? hebu tuongelee swala la ndoa wengine husema ndoa ni bahati, wengine husema ndoa ni zali, na mambo mengine mengi tu..
lakini kwa upande wangu naamini ndoa inastahili kwa kila mtu na sio bahati wangapi tumewaona wanaoa na kuolwa na miaka 40 hata 50? katika vitabu vya Mungu vinasema Mungu alimuumba mwanaume na katika mbavu zake akamtoa mwanamke na kama ni hivyo basi kwa kila mwanamme kuna mwanamke ni muda tu wa yeye kutokea.
lakini nashangaa siku hizi wanaume na wanawake wengine wameoa lakini bado wanataka cha pembeni sasa ukienda kuchukua mwanamke sio wako huyo mume wake atampata lini???
wenyewe waitwa "vidumu" ndio wanawake na wanaume wanavyojidangaya kama wewe kidumu basi huyu mwanaume ama mwanake wako anayekufanya kidumu atakuwa hakupendi kwanini usingewekwa ndani ukawa wa ndani ama tank kama wanavyoitwa wanaume ama wanawake wenye ndoa..
wapembeni atabaki kuwa wapembeni siku zote na utakapo pata shida na magonjwa hatakudhamini cha zaidi atakuacha na kufwata mwengine kilichobaki ni tuheshimu ndoa zetu na wale tuliowachagua kwakuwa ndio watakuwa nasi kwenye shida na raha kwani ni wao tuliowachagua na kuapa nao kanisani.....
mume wa mtu ama mke wa mtu kuwa mchumba wa mtu mwengine inahusu???
hilo suala la ugonjwa hata wenye ndoa watalipata kutoka kwa wenza wao ambao hawajatulia. muhimu kama una ndoa yako na mumeo/mke anatoka nje tafuta reson may be jamaaa kagundua sasa kuwa haukuwa chaguo lake alikurupuka. kwa hiyo wenye ndoa angalieni hilo na unaweza kuwekwa ndani na mr anarudi saa 8 usiku haina maana kwa kweli na mapenzi hapo hakuna ila ni kuvuta siku tu bora tu upo katika ndoa. mh: yatanishinda mie
ReplyDeletehaijalishi kama mwenzi wako anawahi kurudi nyumbani ama hawai point tunayoongelea hapa ni kwamba wa ndoa ni wandoa tu... huyo anayerudi saa nane usiku angeona huko nje ni pazuri kuliko ndani basi angelala huko milele lakini kwasababu anarudi nyumbani kwake wadau lazima mkubali hakuna zaidi ya aliyewekwa ndani..
ReplyDeleteni kwli yule wa ndani ni ndio wa zaidi ndo mana hata akitoka huko akwendako lazima atarudi and luvy dovey lazima atakupa.... nafasi ya wa ndani haiwezi badilika hata kama jamaa anaenda akokwenda,... wa ndani anaitwa UTAKUJA (hiyo ni aka tu)....
ReplyDelete