▼
Wednesday, May 12, 2010
MNENE LAKINI BADO MZURI
HII NI KWA WANAWAKE WOTE WANAOJIHISI NI WANENE NA HAWAPENDEZI...
swala la unene limekuwa kubwa sana hapa duniani, tunasikia na kuona kwenye vyombo vya habari watu wanatumia madawa ili wakonde wengine hata kwenda hospitali kupunguza sehemu za miili yao.
lakini cha kushangaza nikwamba watu hukimbilia wembamba lakini hawataki kukubali kwamba hata ukiwa mnene unaweza onekana mzuri kwa kujivalisha nguo zitakazokupendeza zisikushike sana mwili kwasababu zikikushika mwili basi utaanza kujisikia hukai vizuri na nyama za mwili wako kujikunja pamoja na nguo na kukufanya ujione mnene na uuchukie mwili wako..
ukiachana na hayo tunajua nguo nyeusi humfanya mtu kuonekana mwembamba japo chini ya umbile lako kidogo basi akikisha hukosi nguo nyeusi pia hutupa ujasiri..
mwanamke yeyote awe mwembamba ama mnene anapojipamba vizuri huonekana mzuri sana hiyo pia ni silaha kubwa.
kwahiyo haina maana kuogopa na kukaa bila raha kisa tunaogopa watu wataongelea unene wetu tunaweza kuwa wanene lakini tukavaa na kujipamba kama hao wenye miili membamba nakuonekana wazuri kama wao na hata mara nyengine kupendeza zaidi yao.
Uzuri hautokani na kuwa mwembamba au mnene jamani,tuache kuwa na kasumba hizi vichwani.Hii dhana ya wembamba kudhani kuwa ni uzuri imewafanya wasichana wengine wajikondeshe mpaka wanatia kinyaa matokeo yake wanakosa hata huo mvuto wanaoutafuta.Mwanamke yeyote akijipenda,kuvaa nguo zinazoendana na mwili wake na kujiheshimu atapendeza tu.
ReplyDelete