Wednesday, May 19, 2010

KWA WALAJI KITIMOTO.....





Nina swali kwa wali wa kiti moto, hivi kuna dada mmoja ameolewa na muislamu ambaye ni swala tano kama wanavyoitwa watu ambao huswali sana, sasa huyu dada yeye ni mkristo hodari sana na mbaya zaidi ni mpenzi sana wahiyo nyama katoliki kama nilivyosikia watu wanavyoiita, huyu dada yeye anadai ya kwamba hawezi kuizcha kula hiyo nyama japo mume wake hali hata siku moja, rafiki zake wengine wanamwambia aendelee kula kwani mumewe hawezi kugundua kwani inaandikwa usoni kama umetoka kukila wanamwambia......sasa yeye anachojisikia vibaya ni pale anapotoka kula na kurudi nyumbani na kumpa penzi mumewe maana mume wake akitaka anashindwa kumkatalia, mpaka imefikia sasa ameamua kumdanganya akisikia jamaa anaanza kuomba yeye anajifanya anausingizi ile mbaya.... anasema amejitahidi sana kuacha kuila lakini ameshindwa... afanyeje?

No comments:

Post a Comment