yani hizi mali hizi siku hizi au ilikua tokea zamani..jamani mpaka namuonea huruma huyu dada huyu dada walizaliwa watatu kwao wasichana wawili na mvulana mmoja
mama yao alifariki na baba yake kuona yupo peke yake kwenye nyumba kubwa akaamua kurudi kijijini kwao kumalizia uzee akawaachia watoto wake nyumba yake kuwa ni urithi kwao nyumba ni kubwa na inauwanja mkubwa tu
mwanzoni wakaa vizuri sana huyu kaka ameoa anakaa hapohapo na mkewe na watoto wake wanne, hao wasichana mmoja kazalia nyumbani tu mtoto mmoja na mwengine pia kazalia nyumbani watoto wawili
huyu kaka majirani wanasema anapenda sana mambo ya kishirikina haswa kuwafanyia ndigu zake ili awadhurumu mali na ukiangalia ni watoto wakike ambao ni wanaishi tu uswahilini na maisha ya uswazi labda hawajui hata maana ya haki za mwanamke na kama kuna watu wanaotetea wanawake kisheria
basi katika wale wasichana wawili mmoja akaamua kuhama na kwenda kupanga mbali lakini upande wake wa nyumba bado ulikuwepo tu, kwahiyo kwenye nyumba akabaki yule msichana mdogo na kaka yake pamoja na familia yake
mdada wa watu huyu alikua hana kazi nyengine zaidi ya kuajiriwa salon, lakini watu walikua wanashangaa yeye ndiye alikua analisha familia yote hiyo kubwa kaka yake hafanyi anabaki tu kuendeleza kujenga nyumba vyumba ili apangishe ikawa hivyo kwa muda mrefu mtaani wakaanza kusema kamfanyia mdogo wake chuma ulete siunajua waswahili tena
basi maisha miaka nenda rudi ndio hivyo kwao watu nje wanasikitika tu na kuongea chini kwa chini mashoga wa shisti wakimueleza anaona wanamsema majungu anaenda kukusemea kwa kaka yake unachambwa kwanzia na kaka mtu mpaka mtoto wao siunajua tena maisha yetu ya uswazi mabibo kwahiyo watu wakawa wanapotezea na kuongea chini kwa chini
ghafla huyu msichana akaumwa sana bila kaka yake kuonyesha mahangaiko yoyote ya mdogo wake ili apone mpaka yule dada yake mkubwa ndio kuacha chumba chake huko alipokua kapanga kuja kumuuguza mdogo wake mpaka alipokata roho
basi msiba ukafanyika watu wakazika maisha yakasonga sasa miezi mitano sasa tokea mdogo wao afe, yule dada aliamua kubaki pale ili amlee yule mtoto mdogo ambaye yupo la kwanza aliyefiwa na mama yake
basi yule kaka mtu hata shs mia hampi yule mtoto, maisha yao wenyewe ya kawaida kinachouma watu mama yake ndiye alikua akiilisha familia ya kaka yake leo hayupo mtoto wake wamemtupa wamemuachia huyo dada yao ambaye na yeye maisha yake ya kawaida sana, ndiye anayekaa naye hata kumsaidia chakula maharage matupu hamna yule dada wa watu akienda kubangaiza huko akipata ndio wale akikosa walale..
halafu juu ya hapo yule kaka akampigia baba wa mtoto njoo umchukuwe mwanao anapata tabu huku anateswa sana baba wa watu kuja mputa kumchukua mwane kwenda naye kwa ndugu zake ila ndugu zake wakamsihi amrudishe kwa huyo mama kwani kwa kumuangalia tu mwili mtoto anaonekana kanenepa na kupendeza kuliko hata mama yake mzazi alivyokua hai...yule mtoto akauridishwa
ndio dada mtu kumuuliza yule baba kwanini umemrudisha mwanao na ulisema huku anapata tabu ndio kuhadithia A mpaka Z yule dada aliumia sana yule kaka alipoondoka ndio kutoka kwenda kumgongea kaka yake kwanini lakini unanitia ubaya hatakama humtaki huyu mtoto ama mimi usinipakazie ubaya na watu wanaoniheshimu
shoga naambiwa mwanamke akanununiwa na nyumba nzima kuanzia baba mpaka watoto wanakaa uwanja mmoja watoto wa baba mmoja mama mmoja lakini hawaongeleshani wala kuombana moto, hata akitaka kibao cha mbuzi anapanda kwetu kwa jirani ama majirani wengine anaomba anakuna anapika
nyumba yule kaka nje kaweka maji lakini huyu dada haruhusiwi kuchota anachota mtaa wa pili huko ya kulipia na akichota kwa kaka yake anatakiwa kulipia kama mtu mwengine
sasa ukaanza ugomvi huyu kaka anamfukuza dada yake kwenye ile nyumba ya marehemu aichukue yeye apangishe, ndio balaa lilipoanza dada yake anamuuliza kwanini upangishe wakati nipo hapa kumlea na kuhakikisha huyu mtoto anapata haki zake alizoacha mama yake
shoga yule kaka asianze kumpiga dadake yani kama kalogwa hivi huyu kaka kampiga sana mpaka akaanza kumkaba sijui alikua anataka kumuaa kamkaba sana kooni basi familia ya huyu kaka inashangilia tu mtoto wake wa kike yupo form two sijui anashangilia muue kabisa baba muue kabisa kakabwa msichana wa watu kujipindua huku na kule ndio kuweza kuporonyoka na kukimbia
kufika juu sasa kwa majirani hoi barazani kwa mama mmoja hivi rafiki yake analia kachafuka akiongea mdomoni anatoka damu ndio huku na kule kumsafisha na kuhadithia kilichotokea
wengine wakamshauri nenda polisi wengine anza kwa mjumbe wakaamua kwenda kwa mjumbe kwahiyo sasa kesi ipo kwa mjumbe...nyumbani kule paka na panya hata salamu hakuna
kisa nini mali ama??? na siye watoto ama ndugu tunaoshadadia leo kwa mwenzio kesho kwako yani kale katoto ningekuwepo karibu ningekazaba mabao maana nimeama uswahilini ila kama kawaida mama shughuli lazima nipigiwe kupewa umbea na yaliyojiri mtaani kama mama mwenye nyumba...
******END*******
No comments:
Post a Comment