Tuesday, December 9, 2014

Tuzungumze...

Jamani wanawake kwanini hizi tv zinatuaribu, kwanini wanawake wengi baada ya kua na mafanikio zaidi ya mume tunaota mapembe Nimeona wengi sana wanalalamikia hili, hebu leo tuliweke wazi

Sijui kwa dini zingine ila kwa wakristu baba ni kichwa cha familia, haijalishi ni masikini,mzee ama mlemavu

Na ndoa ni sacrament takatifu kutoka kwa MUNGU inatakiwa kuheshimiwa na watu wote, sasa kwanini mwanamke unashindwa kumuheshimu mumeo kisa unacheo kuliko yeye, kila nchi unaenda wewe au kwa vile raisi wa nchi ni rafiki yako au unapokea mshahara mkubwa kuliko mumeo

Wengi hawatambui laana za ndoa huja kwa kila aina hata hii pia, unategemea unavyomfanyia hivyo mumeo akaukunja moyo wake kwa masikitiko ndoa itakuwepo hapo??

Tena wanawake wengine wanadiriki kabisa kusema mbele za watu mimi ndio namuweka mjini baba nanuhii, umuweke mjini wewe MUNGU?? Hujui kama mafanikio yako yeye pia kachangia hata kwa kukaa kimya ulivyokua unamrudia saa tano au sita za usiku ukisema umetoka kupiga madili

Labda kitu kimoja wanawake hawakijui humuweki mwanaume mjini ila katika ndoa za watu weusi dunia nzima baba ni kichwa mama ndio mlezi na kiongozi wa familia, familia itasimama imara mama akiwepo na akijua kuiongoza vyema kiafya,kiuchumi na kimaendeleo

Ndio kabisa nakubali kuna wanawake wengine maendeleo zaidi yamekuja kwenu baada ya wewe kuolewa, lakini kumbuka bila wewe kuolewa labda huko ulipokua ama ungeenda ungeenda kuzima baraka zako badala ya kuziwasha nyota yako izidi kuwaka

MUNGU alikua na uwezo wa kukupa mwanaume mwengine yoyote awe mumeo lakini akaamua akupe huyo baba ndio wako, sasa kwanini umnyanyase,umdharau,umdharilishe

Kama hana kitu kwanini usitumie hela zako na kipato chako kumuinua, akaonekane na yeye kama unavyoonekama wewe

Na siri za ndani shoga hazitolewi nje, hata kama mafanikio ni yako usijitape muache baba awe baba, ili asimame umpe nguvu na yeye atafute zaidi na hata kama hana afurahie unayompa kwasababu unampa kwa heshima na kumjali

MUNGU awabariki wamama wote wenye wame zao mkawalee na kuwatunza kama jinsi MUNGU atakavyo, hivi vitu vya duniani visikupe kichwa na mabavu ukasahau wewe ni nani na nafasi yako kwenye ndoa yako

......END.......

No comments:

Post a Comment