JAMANI WANAWAKE TUWE NA KAWAIDA YA KUCHEKI AFYA ZETU KWAKUWA MIILI YETU INA COMPLICATIONS NYINGI SANA HASWA ZA AFYA UKIJIGUNGIA MAPEMA UNAPONA NA KUTIBIWA ILA UKICHELEWA UNAWEZA KUFA
KUNA DADA MMOJA HIVI HUKU MABIBO KWETU HUYU DADA ALIOLEWA NDOA YAKE INAMIAKA KUMI ILA HAINA WATOTO
HUKU NA KULE KUTAFUTA MTOTO LAKINI HAKUWAHI KUFANIKIWA KUPATA MTOTO
BAADAE AKAPATA SIJUI DAWA GANI AKAANZA KUBEBEA MIMBA LAKINI MIMBA KILA IKIFIKISHA MIEZI SABA INATOKA YANI ANAZAA KABISA MTOTO AMEKUFA
AMESHABEBA MIMBA NA KUZAA WATOTO WA KAFA WATOTO NANE
HAKUKATA TAMAA ALIKUA ANAAMINI IPO SIKU MUNGU BABA ATAMPA MTOTO AKIWA HAI NA YEYE ATAITWA MAMA, ATAFICHIKA NA AIBU YAKE YA KUTOPATA MTOTO
KUMBE ALIVYOKUWA ANAPATA HIZI MIMBA NA WATOTO KUFA MADAKTARI WAKAMFANYI UCHUNGUZI WA KIAFYA KWANINI KILA MTOTO ANAKUFA NDANI YA MIEZI SABA WAKAGUNDUA ALIKUWA NA UVIMBE TUMBONI
HAYO MAUVIMBE NDIO YALIKUWA YANASHINDANA NA WATOTO SIJUI MADAKTRARI WALIO HUMU LABDA WANAJUA KWAHIYO MIMBA ZILIKUA HAZIKAI MPAKA MIEZI TISA, NA ALISHAURIWA KUTOBEBA MIMBA NYENGINE MPAKA HAYO MAUVIMBE YATOLEWE
LAKINI SIJUI NI UOGA, SIJUI NI KUPUUZA, SIJUI NI KUKOSA HELA YULE DADA HAKUTOA ULE UVIMBE MATOKEO YAKE MWAKA JANA MWEZI WA KUMI NA MBILI AKABEBA MIMBA NYENGINE
JUMAMOSI ILIYOPITA AKAZIDIWA SANAAA YANI SANA NDUGU ZAKE WANASEMA HAWAKUWAHI KUMUONA KAZIDIWA NA KUUMWA KAMA ALIVYOUMWA MIMBA HII KWENDA HOSPITAL KAMA MIMBA ZILE NYENGINE AKAZAA MTOTO AMEKUFA
ALIPOMALIZA KUZAA BAADA YA NUSU SAA ALIANZA KUTAPIKA NA KUISHIWA NGUVU HUKU DAMU NYINGI SANA ZIKIMTOKA UKENI NDANI YA NUSU SAA BAADAE ALIFARIKI
MASIKINI YULE DADA MUNGU AKAMBARIKI YEYE NA WATOTO WAKE MAHALI WALIPO.
****END****
No comments:
Post a Comment