BASI BWANA WAWILI HAWA WALIOONA NDOA YA KIISLAMU, NA MIAKA MIWILI YOTE HAWAKUBAHATIKA KUPATA MTOTO
YULE MWANAUME SIJUI NI KWASABABU YA MAWAZO KWAMBA MKEWE HAJAZAA NA WENZAKE KUANZA KUMCHEKA NA KUMPA MANENO YA KEJELI AKAANZA KUWA MLEVI YANI AKAWA MLEVI WA KUPINDUKUKIA
BASI BWANA KUMBE MKEWE ALIKUWA ANA JINI AMBALO LILIKUWA LINAMFANYA ASIZAE MPAKA ATAKAPOTEKELEZA MASHARTI ANAYOTAKIWA KUFANYA NI KWAMBA LILIKUA LINATAKA YULE MAMA AWE MGANGA
BASI WAKAWA HIVYOHIVYO WANAISHI MARA IKAANZA KIPINDI YULE MAMA AKAWA ANAPANDISHA MAJINI YANI AKIPANDISHA MAJINI ANAFANYA VURUGU SANA NA KUDAI MBUZI ICHINJWE ILI ANYWE DAMU
KWAKUWA WALE FAMILIA YAO NI YA MAISHA YA CHINI SANA MUMEWE ASINGEWEZA KUMCHINJIA MBUZI KILA JINI LIKIPANDA, NA LILIKUWA LIKIPANDA LINAMZINGUA SANA MUMEWE MPAKA MWANAUME ANAKOSA AMANI NDANI YA NYUMBA YAKE
BASI BWANA WAKAWA WANAISHI HIVYO MPAKA MIAKA MITATU YA NDOA YULE MUME AKACHOKA SASA NA ILE HALI AKAENDA KUONGEA NA MASHEKH WAKAMSHAURI AONGEE NA HILO JINI PINDI MKEWE ATAKAPOLIPANDISHA TENA
BASI BWANA SIKU JINI LIKAPANDA YULE JAMAA AKAANZA KUONGEA NALO KWAMBA WEWE NI NANI NA UNATAKA NINI KWANINI MARA KWA MARA UNAMPANDA MKE WANGU
LILE JINI LIKAMWAMBIA KWAMBA HALIPO HAPO KUMDHURU MKEWE BALI LINATAKA MKEWE ATAKELEZE MAJUKUMU YAKE AMBAYO HATAKI KUTEKELEZA NA NDIO MAANA MAISHA YAO YAPO HIVYO YALIVYO LEO
BASI YULE BABA AKASEMA NATAKA NIKUONE WEWE JINI NDIO NITAAMINI HAYO USEMAYO NA KAMA KWELI HAUTAKI KUTUDHURU, YULE JINI AKAMUULIZA TENA JE KWELI UPO TAYARI KUNIONA YULE BABA AKAMWAMBIA NDIO
BASI ILIKUA IJUMAA LILE JINI LIKAMWAMBIA YULE BABA SAWA MIMI NA WEWE TUTAONANA ALHAMIS IJAYO, KATIKA KILE CHUMBA CHAKO KIMOJA AMBACHO HALALI MTU NENDA KATOE KILA KITU, KIFANYIE USAFI KIBAKI KITUPU HALAFU ALHAMISI MIDA YA SAA SITA NITAKUJA..UKISHAMALIZA KUFANYA USAFI UCHOME UBANI NDANI NA UKAE KATIKA KONA YA CHUMBA
BASI YULE BABA AKAKUBALI ALHAMISI ILIVYOFIKA VITU VYOTE VIKATOLEWA PAKAFANYIWA USAFI MIDA YA SAA TANO YULE BABA AKASEMA NGOJA NIANDAE MAPEMA AKAANZA KUCHOMA UBANI MULE NDANI AKACHUKUA MKEKA WAKE NA AKAUTANDIKA KAMA ALIVYOELEKEZWA KUFANYA NA LILE JINI
ILIPOFIKA SAA SITA KASORO YULE KAKA AKAENDA KUKAA KAMA ALIVYOELEKEZWA BASI SAA SITA ILIPOFIKA MULE NDANI KULIKJAAA UPEPO MKALI SANA NA BAADA YA HUO UPEPO PAKAJAA NYAMA
MINYAMA MIBICHI IKAJAA NA KUZIDI KUJAA IKABAKISHA TU ILE SEHEMU ALIPOKUA AMEKAA YULE BABA MARA NDANI YA ILE MINYAMA KIKATOKA KIBICHWA KIDOGO KAMA SIZE YA NGUMI YA MKONO WA MWANAUME NA KUANZA KUMUONGELESHA HUYO BABA KWAMBA NAAM NIMEFIKA LEO KUONANA NA WEWE
YULE BABA KUONA AKAZIMIA HAPOHAPO HAKUZINDUKA TENA MPAKA ALIPOZINDUKA AKAJIKUTA CHUMBANI KWAKE KITANDANI KWAKE MASHEKH WAKIMSWALIA
NDIO KUANZA KUHADITHIA KILA KITU NA MASHEKH KUMSHAURI YULE MWANAMKE KUFWATA ANAYOTAKIWA KUFANYA, KWELI YULE MAMA AKAANZA KUTIBU WATU KIGANGA NA YULE MUMEWE POMBE AKAACHA KWANZIA SIKU HIYO NA SASA WANAWATOTO WAWILI..
*****END****
No comments:
Post a Comment