basi bwana kuna dada mmoja anamsichana wake wa kazi, huyu msichana wa kazi kama anamiaka 17 au 18 hivi
amekaa naye ni miezi mitano sasa hivi yule mama anasema, mwanzoni huyu dada alivyokuja alikuwa msichana mzuri sana yani mchapa kazi sana dada wa watu si ndio akasema kweli hapa nimepata msichana wa kunilelea mwanangu
basi na yule mtoto akawa anampenda sana yule dada mpaka yule mama akawa anamruhusu mtoto kulala na dada chumbani kwake na asubuhi dada akiamka anamuandaa mtoto anamfanyia kila anachohitaji kama kuoga na kumlisha yani alikuwa anaimudu sana hiyo familia
sasa huyu mama ni mlokole anasali kwa Mwingira siku zote huwa akitaka kwenda kanisani anaenda na mtoto anamuacha dada nyumbani
Jumapili moja akaamua hapana leo nataka twende na dada kanisani, basi jumamosi akamwambia dada MUNGU akipenda kesho jumapili nataka twende wote kanisani...
dada akamwambia mama mimi sipendagi kwenda kanisani halafu hilo kanisa lenu mnaenda asubuhi mpaka saa kumi kwakweli mimi siwezi huwa naboreka mapema nitashindwa kuvumilia mpaka jioni
yule mama akamwambia hapana kule kunakuimba na kuabudu yani hutaona hayo masaa kama ni mengi sio muda wote tu tunasoma Biblia dada akakaa kimya kama dakika tatu halafu akamjibu dada yake sawa ataenda
yule mama yeye akaanza kujiuliza yani hata siku moja sijawahi kusikia mtu ni mvivu wa kwenda kanisani kukaa tu na kusikiliza Neno huyu ndio wa kwanza, akaguna tu kimoyomoyo akayaacha hapo
kawaida huwa wanamtindo wa kuandaa nguo zao za kanisani jumamosi basi wote wakatoa nguo zao dada akazipiga pasi tayari kwa kesho yake kwenda kanisani
basi bwana wakalala kwa uwezo wa MUNGU asubuhi pakakucha mama akaamka ili aanze kuandaa chai ili wanywe waende kanisani, dada yeye hua akiamka hizi siku za Jumapili anamuandaa kwanza mtoto halafu ndio wanywe chai waondoke
basi mama kuamka anashangaa mbona dada hayupo yani mpaka saa mbili kasoro hajaamka wakati kanisani wanaenda saa tatu, basi akaamua kwenda chumbani kwa dada kuwaamsha dada na mtoto
akaanza kumita dada, dada, dada mmhhh dada haamki akasema yani huyu naye anausingizi mzito ngoja kwanza nimuamshe mtoto halafu nitamrudia akamuamsha mtoto mwanaye akaamka mara moja akaenda sebleni
akaanza tena kumuamsha dada dakika kumi nzima dada hajaamka mmmhhh sindio kuanza sasa kutetemeka huyu mtoto wa watu amekufa ama nini??
basi yule mama ndio kuanza kuchanganyikiwa mtoto wa watu tena sijui itakuwaje ndio huyo kutoka mpaka kwa jirani yake nyumba ya jirani kumueleza
hao wakaongozana mpaka kwa mjumbe kwenda kumueleza basi wakarudi nyumbani kwa huyo dada kufika pale amsha amsha na wewe wapi yule msichana wa kazi hakuamka
basi yule mama wa jirani wakaenda kwa mzee wa nyumba kumi kumueleza yaliyojiri hao wote kuelekea mpaka nyumbani kwa yule mama kwenda kujionea
kufika kule amsha amsha ikaanza tena wapi yule msichana hakuamka..mjumbe akaamua kwamba wakamuite shekh wa msikiti wa karibu aje kumsalia lakini yule mama akasema labda wamtafute mchungaji
Mjumbe akamwambia wewe unajuwa mchungaji hapa karibu yule mama akamwambia hapana mjume akamwambia kwahiyo huyu mtoto wa watu afe hapa wakati unamtafuta mchungaji??? basi wakakubaliana wamuite shekh
wakati wanaenda kumuita shekh na kumuhadithia ndio sasa kwenda kwa yule dada kufika pale wakamkuta yule msichana bado kalala vilevile shekh akaanza kusoma kisomo nadhani ameshawahi kukutana na kitu kama kile maana alivyomuamsha tu mara moja akaanza kusoma kisomo
kisomo kikaanza shekh wa watu akawa anasoma anasoma mara yule msichana akaamka kwa kushtuka kama kashtuliwa hivi au kamwagiwa maji ya baridi usingizini cha kwanza kufanya ni kukimbia mpaka nje
ndio wale nao wakaanza kumkimbiza sasa ndio wakina siye wamtaa kuanza kushangaa watu wakajaribu kumkamata mpaka wakampata shekh akasema atulizwe chini akakaa na akaanza kuombewa tena
basi wakaanza kumkimbiza wote wanne, ndio nje watu wanashangaa kwanini wanamkimbiza basi wakasikia mkamate huyo watu wakamkamata shekh akasema akalishwe chini na kisomo kikaendelea
wakamsomea basi watu wakawa wanajaa pale shekh anaendelea tu kusoma mpaka yule msichana alivyotulia
shekh ndio kuanza kumuulia wewe jina lako nani akasema Stella kwanini ulikuwa huamki ulivyoamsha yule dada akasema mimi ni mchawi na nimerithishwa na bibi yangu
huwa naonekana mchana tu usiku huwa naondoka naenda kwa bibi iringa halafu narudi asubuhi kuendelea na kazi zangu nyumbani kwa dada
akaulizwa unaondokaje akasema usiku nikiwa nimelala naondoka pale kitandani naacha tu mwili wangu ukiwa umelala na mtoto lakini mimi huwa sipo hapo
shekh akamuuliza umeshawahi kuwadhuru hii familia, yule msichana akasema hapana kwasababu dada na mwanae wanakaa na mimi vizuri ila siku mbili nilishawahi kwenda huko kwa bibi na mtoto lakini hawakumfanyia kitu nilimuacha tu anacheza mwenyewe sisi tukiwa tunakunywa damu
shekh akamuuliza huwa mnakunywa damu ya nani, akasema ya wale wanaokufa makaburini wale wapya ambao wanazikwa leoleo lakini hatujawahi kumpa mtoto damu nilimuomba bibi tusimdhuru mtoto huyu kwani wananipenda sana
shekh akamuuliza sasa mbona leo ulichelewa kurudi kutoka kwa bibi
yule dada akamwambia kwasababu dada aliniambia nitaenda kanisani ndio maana nikachelewa kurudi baada ya kumuhadithia bibi akasema nisithubutu kwenda maana watatuua watumalize nami nikakubali kwasababu bado namuhitaji bibi yangu yeye ndio kila kitu kwangu wazazi wangu walishafariki siku zote naishi naye
basi bwana yule dada akamchukuwa yule msichana na kumuomba kwamba kwavile hataki kwenda kuombewa kanisani basi achukuwe tu vitu vyake aondoke basi yule dada akachukua kila kilichochake asubuhi ileile akaenda kupandishwa gari linaloelekea iringa na ndio ilikuwa mwisho wa yule dada
Yule mama na mtoto wake ndio kwenda kanisani kutoa ushuhuda na kuombewa kupewa kinga, watumishi wakaenda kwenye nyumba ya huyo dada na kuifanyia maombi pamoja na kuimwagia maji ya baraka...
********END********
tobaaaaa majanga
ReplyDelete