Monday, October 7, 2013

nitafundisha gubu la ndugu wa mume kwa masomo mawili tofauti kwanza yanayosababishwa na ndugu wa mume kwa ajili ya wanaume kujifunza na pili tunayosababisha sisi waolewaji ili mlioolewa na mnaotaka kuolewa mjifunze...NAANZA NA SISI WAOLEWAJI

jamani ndio tunajua ma wifi na ndugu wa mume wanamagubu hatari tena wakiungana na kuamua kumpindua akili mumeo shoga ndoa huna

lakini magubu mengine siye ndio sababu, nitafundisha kwa mifano kuna dada mmoja alinipigia simu akataka nimshauri kuhusu wifi yake aliyeolewa na mdogo wake

huyu dada akaniambia yani Rose, wazazi wetu walivyokufa hakuna aliyekua anailea familia yetu kama mimi, mimi ndio nilikuwa kila kitu kwa ndugu zangu nilihakikisha wanasoma, wanavaa, wanakula na kila cha muhimu walichohitaji niliwapa

nilikuwa najinyima sana ili wadogo zangu wasikose kitu, sikuwa nimesoma sana na kazi ya kulipwa mshahara mkubwa sina nilitafuta mpaka wame za watu watu wazima wanihonge hela tu ili ndugu zangu wasipate shida

Rose sisi ni waislam na niliolewa ndoa ya kwanza mume wangu alikufa akaniacha na mtoto wa kike ambaye yupo form 1 MUNGU akanibariki nikapata mwanaume mwengine akanioa nikazaa naye mtoto wa kiume ambaye yupo darasa la tatu sasa

kama unavyojua matatizo na raha za ndoa mimi na huyu mume wangu wa pili hatukudumu kwa vituko vyake alivyokuwa ananifanyia nikaamua tu kuomba talaka yangu akanipa nikaachana naye na kuishi kivyangu na wanangu

Rose, huwezi amini ndoa ya mdogo wangu nilihangaika nayo sana wifi yangu nguo yake ya harusi mpaka ya sendoff nilimpa mimi kwasababu huwa nauza nguo za masherehe maana mwanzo tulishibana sana na wifi yangu na nikamchukulia kama mdogo wangu

wala sikumchukulia kama wifi yangu na kwakuwa na yeye wazazi walishakufa anaishi na dada yake nilimpenda sana kama mdogo wangu nilijua ni uchungu gani anaopitia kukaa bila wazazi

basi bwana wakaoana vizuri siye waislam nikaenda kumpikia saba siku zikaenda miezi mitano baadae ndio kilitokea kitu ambacho nilishidwa 

 watoto wangu wanapenda sana kwenda weekend kwa mjomba wao wanaenda ijumaa na kurudi nyumbani jumapili ili wajiandae kwenda shule jumatatu

walifanya hivyo tokea alivyooa na nilijua ni jambo la kawaida maana walifurahi sana mwanzo ikifika ijumaa kwenda kwa mjomba wao maana pale walipopanga kuna wapangaji wengine wanawatoto rika lao kwahiyo huwa wanaenjoy sana kucheza nao

kumbe wifi yangu hakupenda na kuchukizwa na kile kitendo cha watoto wangu kwenda kwao ijumaa akamwambia mumewe kwamba hataki watoto wangu wawe wanaenda weekend wakija wasalimie tu na kuondoka

mara ya kwanza mdogo wangu alijua ni utani tu au labda waligombana sasa mke anataka kumrusha roho na watoto wa dada yake lakini kweli siku zilivyozidi kwenda wifi akawa anakasirika ikafika sehemu wanangu wakienda hawapewi hata chakula mpaka mjomba wao akija ndio awanunulie chips wale warudi kwangu au walale asubuhi awarudishe

na cha kushangaza zaidi akapiga marufuku kabisa hata ndugu yeyote wa mumewe kukanyaga nyumbani kwao hataki kufwatwafatwa

akawa anamwambia mumewe kama ulikuwa unataka kukaa na ndugu zao si ungewaoa hao ukawaweka ndani sasa wanakujakuja kulala nini hapa sitaki tena hata kuwaona waje kulala hapa na kusalimia sio kila mara mtu anakuja hapa waje kwa mwezi mara moja

mdogo wangu akanipigia simu dada nimechanganyikiwa hivi ni mfanyaje huyu mwanamke, ndoa yenyewe bado changa lakini hataki kuona ndugu zangu yani wewe uliyenilea mimi na mdogo wangu msije hapa kisa mwanamke ATAONDOKA

ni kamwambia wala hamna haja kuvunja ndoa yenu kisa wifi hataki ndugu wa mume sisi hatutakuja kwako wewe ukituhitaji unapajua kwetu lakini naomba mkeo akipata tatizo lolote lile usijaribu kunitafuta muache akae nalo mwenyewe na alitatue mwenyewe..

basi siku zikaenda wifi akapata mimba ikafika miezi sita mimba ikatoka tena akazaa kabisa kwa kusukuma lakini mtoto akawa amekufa wala sikukanyaga si amesema tusifike

akabeba tena mimba ya pili ikafika tena miezi sita mimba ikatoka ya kwanza mtoto wa kiume ya pili mtoto wa kike

akabeba mimba ya mtoto wa tatu tena ikatoka naona sasa amechoka kubeba mimba matatizo yote hayo wala sijakanyaga wala kupiga simu

mdogo wangu anaumia kupoteza watoto naona akawa amechoka akaamua kutafuta wa kutolea mawazo nje kwa bahati nzuri au mbaya yule mwanamke akapata mimba na amezaa mtoto wa kiume

kwa nyodo zake wifi hata siku moja hatujasubutu kumwambia na tumemtenga sasa hivi anashinda kwa dada yake jioni anarudi kumpikia mumewe mume mpaka muda anaotaka kurudi ukifika anarudi, kula na kulala

mdogo wangu anasema anataka kumuacha hata kama anampenda mapenzi yote yanaanza kuisha kwasababu hawezi kukaa na mwanamke ambaye hapendi ndugu zake haswa dada yake aliyemlea

na kwakuwa dini yetu ya kislam inaruhusu kumpa mkeo talaka na kuoa tena basi atamuoa yule msichana wake wa nje ambaye amemzalia mtoto

************END************

SASA WEWE MTOTO WA KIKE UNABARIKIWA KUOLEWA HALAFU UNAENDA KUCHEZEA NDOA YAKO KWA ROHO YAKO MBAYA!!!!!

TATIZO WANAWAKE WENGI MNAVYOOLEWA AMA MNAPOTAKA KUOLEWA HUWA MNAINGIA KWENYE NDOA NA MAONO MENGI MABAYA KUHUSU WAKWE ZAKO KISA TU UMESIKIA STORY ZA MARAFIKI ZAKO WALIOOLEWA KABLA YAKO WAKATESWA NA MAWIFI NA MAMA WAKWE

AMA UMEONA JINSI MASHANGAZI ZAKO WALIVYOMFANYIA MAMA YAKO BASI NA WEWE UNAJIANDAA KWAMBA UKIOLEWA MAWIFI ZAKO WATAKUKOMA

NA KWENYE HIZI KITCHEN PARTY MA MC NA WATOA MADA WANAKAZIA KABISA KWAMBA MAWIFI WANA GUBU NDIO KUNA AMBAO WANAGUBU LAKINI MBONA HATUFUNDISHWI KWAMBA NA SISI PIA TUNAGUBU TUNAPELEKEA MAWIFI NA MAMA WAKWE ZETU NAKWAMBIA NITAKUWA NAWAFUNDA NYIE MPAKA MPATE AKILI KWENYE NDOA ZENU USIFUNDWE NA MIMI HAPA UKAACHIKA NITAKUCHAPA VIBOKO

MTOTO WA KIKE UNAPOOLEWA WEWE NDIO UNATAKIWA KUWA BALOZI WA UNAPOENDA TENA BALOZI MWEMA WALE HUWAJUI HAWAKUJUI WAMELEWA KWA TABIA ZAO UMELELEWA KWA TABIA ZENU BASI UNATAKIWA KAMA MKE KUANGALIA YALE MAZURI YAO NA MAZURI YENU NDIO UKAYALETA NYUMBANI KWA MUMEO NA KWA WAKWE ZAKO

KAMA BABA YAKO ALIZAAGA NJE HUKO MAMA YAKO AKAWA ANAWATESA HAO WATOTO USILETE MATATIZO YENU KWENYE FAMILIA NYENGINE UNAPOOLEWA KILA KITU KIBAYA CHA NYUMBANI KWENU UNAACHA PALE HOTELINI MNAPOTOKA HONEYMOON KWENDA NYUMBANI KWENU NA KUCHUKUA MAZURI TU

MUMEO LEO AMEUMWA HOI WEWE UNAWEZA KWENDA KUMFUTA HAJA USIKU ASUBUHI NA MACHANA KILA SIKU ATAKAZOKUWA AMELAZWA HATA KAMA MIEZI SABA UNAWEZA WEWE, SASA HAPO SI NDIO NDUGU WA MUME WANAPOINGIA KUKUSAIDIA AMA UTAMUITA DADA YAKO AKAMSAFISHE SHEMEJI YAKE AMSHIKE SHIKE NA TAULO NA MAJI UUMENI NDIO FURAHA YAKO ALAAAAA NITOLEE WAZIMU HAPA

MTOTO WA KIKE HATA CHAKULA KUWAPIKIA NDUGU WA MUME HUWEZI HELA ATAFUTE MUMEO WEWE KUZITUMIA HUTAKI UNAAKILI WEWE, KUPIKA KWANI NI DAKIKA NGAPI HATA LISAA HALIISHI WATU UKAWAKALISHE NJAA KISA ROHO YAKO MBAYA TENA WATOTO WADOGO

UNATEGEMEA MUNGU ATAKUPA NA WEWE WATOTO KAMA WA MWENZIO HUWAPENDI??? JAMANI WANAWAKE MBADILIKE

NDOA INATAKA AKILI YAKO NA AKILI YA MOYO UUNGANISHE PAMOJA SIO UNATUMIA YA KICHWANI YA MOYO UNAWAACHIA NDUGU ZAKO HAO NDUGU ZAKO WANAWEZA KUKUPA ANACHOKUPA MUMEO WEWE MBONA HUKUBAKI NYUMBANI UKAKAA NAO MPAKA KUFA

NA KWATAARIFA YENU WIFI UKIMCHUKIA NA YEYE ATAKUCHUKIA MBONA MIYE NAKAA NA MAWIFI ZANGU LAKINI LETU MOJA MUME WANGU HAWEZI KUMUULIZA WIFI YANGU KITU KUHUSU MIMI MAANA ANAJUA LAZIMA ATADANGANYWA KWA WIFI KUNITETEA TULIVYOSHIBANA

UNAPOOLEWA JUA KUISHI KAMA PANYA UNAKULA NA KUPULIZA...JUA KUISHI NAO KWA MAZURI WAKIKULETEA UBAYA UNAWACHAMBA LAKINI UZURI WAKO UTATAWALA WATARUDI TU KWENYE HIMAYA YAKO MAANA WANAJUWA BILA WEWE HAWAWEZI..

IFIKE SEHEMU SIKU UKISAIFIRI WANAUMWA KWA KUKUTAKA URUDI HARAKA ...EBOOOOOOO

MJIFUNZE WATOTO WA KIKE


1 comments: