Maombi ni muhimu sana unapokuwa kwenye mahusiano. Wengi wanajisahau wanapokuwa hawajapata mchumba wanaomba usiku na mchana tena kwa kufunga lakini wakishakuwa kwenye mahusiano tu basi maombi yanawekwa kapuni. Kumbuka shetani yupo kupinga kila jambo jema la mtu wa Mungu. Unapolala usingizi yeye ndiye yupo kazini akivuruga mahusiano yako.
Unakuta wengi wanalalamika mahusiano yao hayaeleweki, wanagombana bila sababu, mara wazazi hawamkubali n.k. Tambua kuwa mambo haya mengi chanzo chake ni shetani, lazima ujue kumdhibiti kwenye maombi. Funika mahusiano yako na damu ya Yesu, omba mwenzi wako akubalike kwa wazazi wako, ombea maelewano kati yenu.
Yaani unapoacha kuomba unampa shetani nafasi kuwavuruga. Omba bila kukoma.
Imeandikwa na: Woman of Christ
No comments:
Post a Comment