Monday, October 21, 2013

katika ndoa kuna fimbo nyingi sana za kuchapiana wewe unaijuwa yako..sikia hii

jamani mwanamke unapopata kazi unatakiwa kuipenda na kuwa na heshima kazi yako isiwe fimbo ya kuchapia watu..

jamani kuna dada mmoja ameolewa yeye anakazi ya ofisini ameajiriwa mumewe kazi hana yani yule kaka naona hana tu bahati ya kupata kazi japo amesoma mpaka diploma

kutokana na maisha kuwa magumu kabla ya kuoa huyu kaka alipata kazi katika kampuni ya ulinzi ambayo ilikuwa inamsaidia anapata hela za kulipa kodi na kufanya mambo yake mengine

yule kaka akafanya kazi hapo kwa muda tu ila kipindi cha kati hapa tukagundua kunamabadiliko sana yani kijana anazidi kunawiri alikuwa amepanga chumba kimoja mara akamuomba mama mwenye nyumba yake anataka chumba na sebule kwakuwa kunampangaji mmoja alikuwa anahama kwenye hiyo nyumba

na akavilipia, mara tukaona ndani kunaletwa makochi, firji na makapeti mmhhh watu wakaanza kujiuliza jamaa kapandishwa cheo???? siunajua uswahilini tena

heeeee mara tukawa tunaona mwanamke anakuja siku za weekend anapika na kupakua na kufanya usafi ndio watu wakaanza sasa maneno ya chini chini

mwanaume kabebwa kapata mwanamke mwenye hela ndio maana kamfanyia hivyo vyote, lakini yule kaka hakuacha kazi yake akawa bado anaendelea nayo masikini sema tu ndio mabadiliko kwa mtu aliyemjua tokea zamani anayaona na kushangaa

ikaenda hivyohivyo mpaka yule kaka kuamua kuoa sasa kumuoa yule msichana kweli harusi zetu za ubwabwa simnazijua tukaenda kuoa ndugu na majirani tukachukua mwali wetu akaja uswazini

shoga mwanamke tena naona akaanza kuona aibu kwamba yeye anafanya kazi ofisini mumewe analinda tena kazi zenyewe za kurudi asubuhi akaona isiwe tabu

akamwambia mumewe acha kazi nakufungulia biashara na kila mwezi nitakuwa nakupa laki moja

ukiangalia ndoa ndio kwanza changa jamaa atafanyaje akaamua kweli kuacha na kusubiri mkewe atakapo mfungulia biashara

kweli yule dada akamfungulia duka yule kaka la kuuza vitu vya nyumbani mchele,sijui sabuni etc

maisha yakasonga lakini siunajuwa siye wanawake tena ni wachache hata baada ya kugombana ukamuheshimu mume wako ukiangalia wewe ndio unayeshika maisha ya nyumbani

basi jana usiku sijui waligombana nini jamani aibu hii yule dada alitushangaza mtaani pale alimtukana mumewe matusi na kumdharilisha sote tukajua kumbe yeye ndio alimuachisha kazi na anamlipa kila mwezi laki

yule kaka wa watu kama mwanaume akawa anafoka yule dada anamtukuna na akamwambia anafunga na duka lake kweli yule dada akachukua kufuli akafunga duka akaondoka zake akamuacha yule kaka pale kwa aibu watu kibao wamejaa

jamani watu roho ziliwauma...yule kaka akaondoka na kuingia ndani sasa sijui mpaka sasa hivi kama yule dada alirudi nyumbani kwake au vipi bado sijarudi mtaani ila kwa habari zaidi nitawaahadithia nikirudi uswahilini

0 comments:

Post a Comment