MUNGU alipomuumba mwanaume katika ubavu wake akamtoa mwanamke, na baadae baada ya yote kutokea akasema mwanaume utakula kwa jasho na mwanamke utazaa kwa uchungu...
uende kazini, ulime, uuze biashara, kondakta au hata dereva wa gari vyote utafanya kwa akili mpaka jasho likutoke ili uweze kutimizia familia yako, na mwanamke usukume kwa njia ya kawaida au uzae kwa operation uchungu ni uchungu maumivu yapo palepale...
Japo kuwa siku hizi wanawake pia wanafanya kazi ili kusaidia na mambo mengine nyumbani lakini isiwe kwamba ni lazima mwanamke awe na yeye anatoa kila siku labda kama baba labda umepata matatizo haupo kazini basi mkeo atakusaidia ila pia sisi wanawake sio vibaya japo hela zetu tukawa tunasaidia na sisi nyumbani mara kwa mara na kama sio kusaidia basi tutumie akili za ziada katika hela tunazoachiwa na wame zetu
nitatoa mfano mmoja jana kuna dada alikuwa analalamika huko mtaani kwetu...
huyu dada ameolewa na ndoa yao bado hawajapata mtoto mumewe anaendesha magari haya makubwa yanayoenda congo, malawi na sehemu kama hizo nadhani mnafahamu
akawa anatuhadithia mumewe akiwa anasafiri wakati wa kurudi anasombelea kila kitu cha nyumbani yani michele, mahindi, nyanya, carrot yani mahitatajo yote ya nyumbani yani nyumbani kwao hakujawahi kuishiwa kitu mpaka chumvi anakuja nazo
kwakuwa madereva wanatakiwa kuripoti kila asubuhi makazini kwao mpaka watakapopata safari yule mama anasema mumewe kila siku akiondoka kwakuwa anajua kila kitu ndani kipo anaacha shs 1000
mkewe kila siku anamwambia mumewe kwamba hela haitoshi mwanaume haelewi kwakuwa kama mpaka maharage na kuku analeta kwanini hela isitoshe wakati vyakupika na mboga zipo ndani
sasa yule dada akawa analalamika kwetu yani sawa mimi siwezi kula nyama maana nyama kwetu nusu 2500, siwezi kulipa taka kila wiki taka tunalipa 500 kila nyumba wala siwezi kwenda salon maana yule mama si mama wa nyumbani shoga na ujuzi hana
yani uswahilini kama kazi huna, biashara huna hata ujuzi pia huna utapata tabu sana omba mumeo awe kaweka stat time nyumbani kwako utashinda unaangalia lakini kama hauna kama nyumba nyingi za uswahili zilivyo utalala wewe mpaka uunge ushoga na kitanda
mimi nikamwambia kwanini usitumie ujanja wa ziada wanawake tulipewa akili ya ziada ambayo haikai kwenye ubongo hiyo hukaa kwenye damu
maana mumeo ndio kashagoma kuacha hela zaidi ya 1000 na wewe unataka upendeze, ule nyama mtaani tukuone, sasa nunua kibubu shoga yule baba anavyokuachia hiyo 1000 kila kitu ndani si kipo jumatatu mchana unabandika maharage jioni kuku ile hela miatano unaweka kwenye kibubu miatano unaweka sehemu yako unapohifadhi hela zako
kwakuw aunakuwa peke yako mchana jumanne akikuachia 1000 miatano weka kwenye kibubu, miatano nyengine nunua mlenda pika ugali na mlenda kaanga na kipande cha kuku akuu unakula bibi
jumatano akikuachia 1000 mia tano kwenye kibubu miatano nunu mihogo kula mida ya saa nne utakuwa umefidia chai na chakula siku zimeenda
alhamisi anaacha 1000 mia tano kwenye kibubu miatano kwenye begi mchana unapika wali kama na kuku jioni na maharage
Ijumaa kwakuwa ndio siku ya kulipia taka akikuachia 1000 mia tano kwenye kibubu, mia tano lipia taka kula utakula kiporo cha jana yake usiku..mpaka usiku ndio upike na siku hii kaanga tu kuku wako na ugali ukate na kachumbari
kwenye begi kule ana 2000 tayari jumamosi akiacha 1000 mia tano kwenye kibubu mia tano kwenye begi kwakuwa na viazi analeta mchana unapika tu viazi vya siku nzima mpaka jioni
Jumapili akikupa 1000 miatano kwenye kibubu miatano kwenye begi mpaka hapo kwenye begi una 3000 unaenda kununua nyama yako robo inawatosha watu wawili inayobaki unaenda kuseti unywele
tena unahakikisha hiyo nyama unapika jioni akiwemo mchana pika wali wako na maharage jioni nenda zako salon seti nywele zako vizuri upendeze ingia jikoni kaangiza pilau lako la haja kata na kachumbari yako tenga mezani nenda kaoge vaa dera lako nywele zako zipo ng'aring'ari kaa mtoto wa kike ule na mumeo
yeye atakuwa anashangaa tu hii budget ya nyama na jinsi ulivyopendeza wewe kimya muudumie kwa mapenzi tele, na huku ile siri ya kibubu unaijuwa wewe mwenyewe mtoto wa kike siku mumeo ka kwama hana hata hiyo 1000 vunja kibubu udumia nyumba yako
hivyo ndio tunavyoishi wake za watu kwenye nyumba lazima uwe na akili ya ziada kama mwanamke usione ndoa mwanaume anapendeza watu wanaamani hata sisi tunamajaribu yetu humo lakini hukasiriki na kuongea ovyo unatumia akili ya ziada
tukivunja vibubu ndio unaona leo sahani zimebadilishwa, labda tumenunua hiki na kile au watoto tumewafanyia hivi ukiwa mke lazima ujue kutumia akili ya ziada iliyo kwenye damu....
basi shoga kaondoka pale ananishukuru kama kawaida yangu dada yako nikampiga dongo nyooooo ulivyotaka kuolewa hukujua kama kuna hekaheka huko kwenye ndoa
Lakini pia wame zetu hebu watambue unapomuoa mkeo umemtoa kwao mtoto kang'aa ndio maana ulipomuona tu ukawa hoi na kutaka kuwa nae sasa kwanini umuoe alafu ukamfuje mtoto wa watu
yani watu wakimuona mkeo wanashangaa loohhh mbona umefifia umekuwa huna nuru bora ulivyokuwa kwa wazazi wako..hii si aibu yako baba hebu jifunzeni kujirekebisha
mtoto wa kike anataka matunzo, mtoto apendeze, eeehhh kila mtu kwenye ukoo wake akaone raha ya mtoto wao kuolewa na wewe uwatamanishe mpaka wadogo zake wa kike na wao watamani siku waje kuolewa watunzwe na wame zao kama dada yao anavyotunzwa na wewe
Eboooooooooo
0 comments:
Post a Comment