Wednesday, September 25, 2013

Mtaani kwetu...

Hahahahahahahahahaha wanaume jamani, kumbe bwana mwanaume mchezo mchafu wa kuwa na mahusiano nje ya mpenzi wake afanye yeye akifanyiwa yeye hata kwa wazo tu ni sumu...ngoja niwape story ya mtaani kwetu

basi bwana kuna huyu baba mtaani kwetu (waislam) samahanini kama nitawakwaza yule baba ni muislam wale wanaovaaga suruali haifiki magotini wanaitwaje sijui...

yani yeye sijui anafanya kazi wapi ila huwa anapitaga mbele ya nyumba yetu anaendesha baiskeli basi kwenye ile baiskeli yake huwa kila siku ya MUNGU anabeba mifuko myeusi hii ambayo tukienda gengeni huwa tunafungiwa bidhaa

basi utakuta kabeba nyanya hizo ndio huwa zinaonekana vingine huwa sivioni siunajua tena ukikaa barazani mwisho utatoa macho uulizwe mama unamatatizo gani mbona unaniangalia sana.

halafu mida yake ya kupita huwa ni saa mbili usiku kila siku ya MUNGU, nimeshamchunguza sana yule baba kila siku ni hivyohivyo nikawa najiuliza sipati jibu ila moyoni nikawa namsifia sana kwamba ni mume bora yani kila siku anakumbuka kubebea familia yake zawadi..nikawa nawaza mkewe atakuwa na raha sana

jana bwana akawa anapita akakutana na rafiki yake ambaye na yeye alikuwa anapita hapohapo si ndio kusimama na kuanza kusalimiana na kujuliana hali.

miye tena shoga kidawa huyoooo nimetoka zangu kupaki gari mtaa wa pili nawaona wale kwa mbali wanaongea nikasema leo nitatembea kama bibi harusi nikifika pale kwao nitadondosha funguo ili tu nizuge nisikie wanachoongea.

basi kama MUNGU vile ile nimefika pale nasikia rafiki mtu anamuuliza shemeji hajambo?jamaa akamwambia hajambo ndio namuwahi hivi nimepelekee vitu vya kupika

basi miye nikajifanya ufunguo nimeokota ukanidondoka tena ilimradi tu nisikie hichooo nilichokuwa namuwazia yule bwana

yule mwenzake akamwambia anha leo unataka akapike vya kuletewa na mume safi sana, jamaa akamjibu hapana miye siruhusu mke wangu kwenda gengeni bwana asije kutongozwa na muuza genge na kupewa nyongeza nikalishwa haramu

hahahahahaha nilitaka kupasuka kwa kucheka nikasonya kimoyoni kumbe wivu tu na vya kula haramu ndio vinakuponza kila siku kubeba vifurushi nilijua unapeleka zawadi kumbe unamtia mkeo adhabu kila siku ya kuanza kupika saa mbili za usiku.

nikaokota funguo zangu huyo nikaanza kucharanga mwendo nifike nyumbani nianze kuwapa watu umbea maana wote kwetu tulikuwa tunamshangaa huyo baba


No comments:

Post a Comment