Nataka niongee na wanawake ambao hawajazaa na wanawake ambao
wanamimba, unajuwa wewe kama mwanamke ni mtu wa thamani sana duniani bila wewe
dunia itakuwa tupu, ni wewe unaweza ukazaa watoto wenye baraka na ni wewe
unaweza ukazaa watoto wenye laana kabla hujapata mimba pindi unapoanza kumjuwa
mwanaume hakikisha mara kwa mara unaombea tumbo na uzao wako utafanyaje huwa
napenda kuwashauri wanawake vyumbani mwao wasikose mafuta ya nazi ama ya olive
oil utayaombea hayo mafuta kwa dini uliyonayo mimi huyaombea na kuyageuza kuwa
damu ya yesu, basi kila utakapokuwa unaombea tumbo lako utajipaka na kuanza
kuongea na MUNGU kuhusu uzao wako kama hujazaa utaomba MUNGU akubariki tumbo
lako likapate kubeba mimba kwamba hatakama kuna wagumba kwenye ukoo wenu lakini
wewe utazaa kataa hali na roho ya ugumba na ukazae tu na mume wako au na
mwanaume MUNGU aliyekupangia kataa kuzaa na mume wa mtu kwani watoto wengi wa
wame wa watu hawathaminiwi wanafichwa hawatambuliki na utakapokuwa umebeba
mimba kila siku asubuhi paka tumbo lako na yale mafuta muombe MUNGU akulindie
mtoto wako kila siku, mwanao akitoka afanane na baba yake au wewe mama yake,
akawe mtoto wa baraka, mvunjie laana zote za ukoo kabla hajatoka, kataa mimba
kuharibika, muombee akija duniani akapate kuwa baraka kwa watu na sio laana,
muombee akawe na akili kabla hajaanza hata kuongea,usisahau kumuombea kuwa mcha
MUNGU maana huo ndio wingi wa maarifa...TUJIFUNZE kuombea matumbo yetu dunia
inaharibika na kubarikiwa kwasababu ya tumbo la MWANAMKE...
No comments:
Post a Comment