Tuesday, March 12, 2013

UKE WENZA AU MUMEO KUWA NA VIMADA KWA SIRI KIPI BORA?

Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa, wanawake wengi wanachukia uke wenza huku wakitoa sababu ambazo kwa upande mmoja zina msingi. Ni wachache sana ambao huonesha kuukubali tena kwa shingo upande kutokana na imani za kidini.
Tunapozungumzia suala la ndoa, tunazungumzia kitu ambacho kimebarikiwa na Mungu. Kuoa ama kuolewa ni moja ya kutekeleza maamrisho ya aliyetuumba.

Binadamu wameumbwa na kuletwa hapa ili wazaliane na kuijaza dunia, kuzaliana ambako kunapatika kwa kufanya tendo la ndoa baina ya mwanaume na mwanamke ambao wamefunga ndoa kanisani ama msikitini.
Zipo ndoa ambazo siku hizi zinafungwa bomani hasa pale waliopendana kuamua kuwa kitu kimoja yaani kuishi kama mke na mume wakiwa na imani tofauti.

Kwa upande wa Wakristo, sheria haimruhusu mwanaume kuoa mke zaidi ya mmoja. Unapofunga ndoa ni lazima ukubali kuishi na mke wako huyo mmoja mpaka Mungu atakapowatenganisha. 
Wengi wamekuwa wakifuata maandiko hayo lakini kutokana na matamanio yao wamekuwa wakijitafutia nyumba ndogo.

Kwa upande wa Waislam, wao sheria inaruhusu mwanaume kuoa wake zaidi ya mmoja ilimradi wasizidi wanne. Kutokana na sheria hiyo, baadhi ya wanaume katika dini hiyo wanalazimika kufanya hivyo huku wakieleza kwamba ni moja ya kufuata suna za Mtume Mohammad. 

Nadhani hakuna ubaya kwa kufanya hivyo kwani kinachofanya kazi ni imani. Imani ndiyo inayonifanya mimi niende msikitini, wewe uende kanisani. Kwa maana hiyo siwezi kukulazimisha wewe uoe wake wawili wakati dini yako inakutaka uoe mke mmoja tu au usioe kabisa.
Ila sasa, utafiti nilioufanya 

umebainisha kwamba ni asilimia ndogo sana ya wanawake ambao wako tayari kuishi maisha ya uke wenza. Wengi ambao hawajaolewa wanaeleza kwamba ni bora wasiolewe kabisa kuliko kuolewa na mwanaume ambaye tayari ameshaoa. 
Hata wale ambao wako ndani ya ndoa, wengi huamua kuvumilia lakini ni wazi kwamba hawasikii raha kugawana penzi la mtu mmoja, yaani kuchangia mume.
 Sababu kubwa wanayoitoa ni kwamba, wanawake wameumbwa tofauti, kimaumbile, kisura na hata suala la kuridhishana kimapenzi linatofautiana kutoka kwa mwanamke mmoja na mwingine. 
Mara nyingi waliooa wake zaidi ya mmoja ni vigumu sana kuwatosheleza wote.

Source:Global Publisher

No comments:

Post a Comment