Monday, March 4, 2013

Lako hilo kama linakuhusu...

Hamjambo..

Jamani leo nataka niongelee swala moja ambalo nahisi limeshamiri sana siku hizi sijui watu wanaona ni fashion kufanya hivyo hivi inahusu nini wewe mwanaume ambaye una girlfriend unamwambia mpaka akubebee mimba ndio umuoe..Inahusu

Wenyewe wanasema eti hawataki kuuziwa mbuzi kwenye gunia kwani wewe mtoto wa nje, mama yako na baba yako si walioana ndio ukazaliwa wewe kwani wao hawakujuwa kama kunakuuziwa mbuzi kwenye gunia???? haipendezi bwana mbadilike tena mwengine mwanamke wake akikataa nakwambia hata kumuacha anamuacha..eboooo

Na nyie wanawake kutaka kujishebedua kubeba mimba bila ndoa eti manasema waowaji hamna kwani unadhani kila aliyeumbwa mwanamke anastahili kuolewa???? hata kwenye biblia inasema kwamba kunawatu wengine mpaka wanaonja umauti hawata oa wala olewa sasa labda wewe ndio mmoja wao halafu bora ubebe mimba uwe unakazi na hela ya kumtunza mtoto sio unabeba tuu kwa vile unajuwa unauzazi basi utabeba mtoto wa kila mwanume kisa kutafuta ndoa na wote wasikuoe unabaki unahangaika na watoto utamkuta mwanamke mdogo kachakaa kisa anahangaika kutafuta hela kuhudumia watoto wake.

Shoga kisa cha kuchakazana ni nini, siku hizi kuna mwanamke aliyechakaa, utachekwa kwa taarifa yako hata uswahilini siku hizi wanawake wanawaka ukisimama naye wewe wa masaki hujui yupi broiler yupi wa kienyeji..endekeza tu kupanua miguu kwa kutafuta ndoa. shauri yako

No comments:

Post a Comment