leo kuna mtu nilikuwa naongea naye kuhusu uzazi wa mpango akaniuliza watoto wangu wamefwatana kwani ni mapacha? jibu ambalo alishangaa kuwa hapana ila niliwazaa jumamosi na jumapili najuwa manajuwa uzazi huo ni upi kwa wengi wenye watoto, ila kwa wale ambao hamjui ni kwamba unambebea mtoto wa kwanza mimba nyengine akiwa bado hajakomaa vizuri, mwanangu wa kwanza alipokuwa na miezi tisa nikabeba mimba ya mwanangu wa pili kwahiyo ukiwaona sasa kama mapacha na mmoja akiumwa asubuhi mwengine anampokea jioni yani wameshakuwa kama mapacha.
Anyways back to my point nikamuuliza kama anamtoto akaniambia anao wawili mmoja yupo la sita na mmoja yupo la kwanza nikamuuliza uliwezaje kukaa muda wote huo maana mimi hapo ningekuwa nimeshazaa kama wanne kama nisingefanya uzazi wa mpango akaniambia kwamba yeye hakufanya kitu cha uzazi wa mpango huu tunaofanya mahospitali bali alitumia mbegu za mnyonyo.
Ndio mbegu za mnyonyo pia ni dawa ya kuzuia kubeba mimba ananiambia alipopata period yake mwezi wa kwanza baada ya kujifungua akanywa mbegu moja na mwezi wa pili akanywa moja na mwezi wa tatu akanywa moja halafu baada ya kila mwaka anakunywa tatu kwa mpigo ndio maana habebi na hajawahi kubeba mimba tokea ameanza kunywa hizo mbegu.
Nikaona hilo ni jambo zuri maana kwa wale ambao wanahofia kunenepa sijui wakitumia uzazi wa mpango wamahospitali basi hii ni njia nzuri ama kwa wale wakulewa mara kwa mara ukasahau kunywa vidonge vyako vya uzazi hii pia ni njia nzuri sana kwao
Sio kwamba kwa sababu ushajuwa unauzazi ndio uzae jeshi inahusu???? haya habari ndio hiyo kama hutaki uzazi wa mpango wa hospitalini kama nilioufanya mimi unaweza ukajinywea tu hizo mbegu maisha yakasonga.
No comments:
Post a Comment