Monday, February 4, 2013

Wame kuelekea Valentine's Day....

Leo nataka kuongea na wame wanaoingia huku kwasababu najuwa wapo wengi na uzuri wengi hao ndio wamewaambia wake zao kuhusu hii blog kwahiyo najuwa ujumbe utawafikia wengi.

Mimi ni mke nataka niongelee hili kwa upande wa mke na pia kwa kujuwa raha na karaha za wame kwenye ndoa, na nitaongelea hili kwa niamba ya wake wote ninaokutana nao katika vijiwe vyetu tukiongelea matatizo na raha za ndoa zetu na tukizidi kupeana moyo na upendo wa kwamba ndoa ni jambo jema na hakuna kuachia katikati tutaenda wote mpaka mwisho wa safari atakapotangulia mume ama mke.

Ndoa nyingi chanzo cha migogoro ni wame, japo nakubali kuna ndoa nyingine wake ndio huaribu ndoa zao wenyewe lakini leo naongelea mume kuwa chanzo cha kuharibu ndoa yake mwenyewe.

  1. Mume unapoondoka asubuhi hujui familia yako imeamkaje lakini bado mke wako kila asubuhi ukiwa kazini atakupigia simu kukujulia hali na kukujilisha wameamka sala, wakati unatakiwa kumjibu kwa upendo unamjibu 'poa'
  2. Mume unapoondoka nyumbani mkeo anapokuomba uache pesa za matumizi unamjibu kwa hasira au bila hasira hujapata hela halafu unarudi saa sita usiku ukiwa umelewa hujitambui hata nyumbani umefikaje
  3. Mume ambaye huachi hela nyumbani mkeo yeye hafanyi kazi akamua kuomba hata kwa ndugu zake ili mradi mle, halafu ukirudi nyumbani unaanza kumpiga na kumsema lazima atakuwa na hawara ambaye amempa hela ya kupika, wakati mkeo anajuwa jukumu lake kama mama lazima baba akiwa hana hela bado akute chakula mezani.
  4. Mume ambaye siku kweli mlikuwa hamna unaondoka nyumbani unaacha 1,000/= mkeo anaumiza kichwa mnakula ugali, na tembele mnalala ukimkumbatia mkeo unamwambia asijali siku mambo yatakuwa mazuri sasa MUNGU amewabariki mambo yamekuwa mazuri humuheshimu tena mkeo humpi hata hela ya kitenge wewe unahonga na kubadilisha mahawara wakula nao hela yako
  5. Mume ambaye unasema unamuheshimu mkeo lakini kila siku unabadilisha wanawake unalala nao kila mara hutambui unamdharilisha na kuharibu agano la ndoa uliloweka kwenye madhabau na wame mtambue chezeeni kila kitu lakini sio agano la MUNGU kwasababu anasema liliofungwa duniani na mbinguni limefungwa sasa wewe ukilifungua usipojuwa kutubu na kumuomba MUNGU na mkeo akusamehe hiyo dhambi kabla ujauonja umauti 'utailipia'
  6. Mume ambaye mkeo anakutimizia kila kitu lakini wewe kwa tamaa zako za mwili kila unapotongoza unasema mkeo hakupi hili anafanya vile ananiudhi hivi wenyewe mnaiita maudhi madogo madogo kutwa nyie huwa mnajiweka sana mbele bila kutaka kujuwa nini la kufanya kuondoa hayo matatizo nyie suluhisho lenu ni kutoka nje ya ndoa na balaa likakukuta ukapata magonjwa unarudi nyumbani na bado mkeo anakuhudumia kwa mapenzi yote na unamuambukiza na yeye hilo gonjwa kwa sababu mke anaamini mumeo wakati wowote akitaka unampa tena bila condom.
  7. Mume ambaye kila siku unampiga mkeo kisa analamika kwanini unaenda njia ambayo sio badala ujitahidi kuishi kwa kuridhishana lakini wewe unamchukulia mkeo poapoa japo umempiga kaamumia ana maumivu ya moyo lakini bado anakuhudumia na kukupenda kama mumewe tena kama hakuna baya ulilomfanyia leo umuhimu wake hujauona ila siku akifunga macho usijejutia hukumpa penzi ulilotakiwa kumpa maana hata ulie vipi hutaweza kumrudisha hata kwa dakika moja. 
  8. Kuelekea valentine's day wewe mume najuwa unajuwa kati ya hayo kuna hata moja ambalo umemfanyia mkeo au baya zaidi ya hayo lakini mkeo hajaondoka, bado anakupenda, kukuvumilia na kufanya majukumu yake ya mke kama anavyotakiwa basi unastahili japo kwa siku hiyo moja mshukuru na umuonyeshe upendo japo kwa siku hiyo moja nawaomba kwasababu naamini mambo anayoyafanya mkeo kero zako na yote anayoyavumilia huyo hawara yako unayemuona wa maana ukimfanyia hivyo amini nakwambia hatakaa kukuvumilia utatupwa huko kwenye dustbin na hivi hakuna kinachowaunganisha zaidi ya mzunguko....TAFAKARI

2 comments:

  1. Nimekupenda sana dada kwa mada yako natamani mume wangu angekuwa anaingia humu ili awe anapata ujumbe kama hivi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mke wangu usijali,nimeimgia humu na ujumbe nimeupata.

      NITABADILIKA.

      Delete