Wakaanga mbuyu waachie wenye meno watafune, leo ni leo sikuache unichimbi wewe utanitambua fisadi usio na haya nakuweka kitimoto kumbe ndio kazi yako jasusi mpekepeke kupita kukaanga mbuyu waachie wenye meno watafune..hehe heiya
chokochoko zako shoga leo tumezibaini nazimwaga zisikie hadharani jungu ulilolikoroga.....unahashua la boga kuzaliwa majanini mbuyu ulizozikaanga unapata tija gani uchonganishi ukome kuyatafuta ya kwetu nakutia tumbo joto..halooooooooo
Namserembua ndani namvuruga akili,anapata mambo moto, je unamaneno, shoga unaswali, je yamekutachi mpenzi wangu haniachi..mkaanga mbuyu waachie wenye meno watafune ni wangu huyu maneno yenu mkaseme pengine hanibanduki huyu amenipenda miye nampandisha malaika ameshapagawa kasahu alipotoka
Nikimwambia nenda..sitaki nitakosa mengi ndio jibu lake bwana..hehe heiya
kwenda kumtonya mimi ninamsaliti bwana mwengine ninaye namfwata msasani, utavuna nini wewe pole yako...tangu leo unituwe bibi.. nipatalo ajuwa yeye siri iliyomtungini si bora useme tu kama wewe wamtaka ya nini kunifitini na bwana kashaamua wala hanipi talaka kwa raha zangu za ndani..hehe heiya
Hapo sasa wenye nyonga zao.........enheee chini sasa hapo enheeee panda juu mchungulishe dirishani apunge upepo..hehe heiya
story story za bwanaangu wewe za kuhusu nini safari safari za mume wangu wewe zakuhusu nini anayoruhusa yangu programu ipo ndani..atauone uchungu umemuona kwa fulani hunirushi roho yangu nampenda mwa ndani..wewe wa gazeti gani
mchakamchaka namchezesha miye kijasho chembamba kinamtoka utamu umemkolea hataki kuniachia..haloooooooooo
Raha ya kunywa uji kuzungusha bakuli bibi...enheeeeee
Tena nasjisifia na kitabu sijammalizia chokochoko zako hatuzitaki umepiga simu sisi tupo fiti...
Kumbe bibi wewe mambo haya umeanza zamani, wifi zangu waambia nina buzi magomeni wanichukie moyoni kama huo sio umbea tuuite jina gani tena wanipakazia eti mimi ni muhuni ewe mwaya wa hisaya aliyokuajiri nani..hapo sasaaaaa wale wambea woteeeeeeee lenuuuuu
Ukiona bibi na bwana wanapendana moyoni roho yako usonona unapekechwa kwa ndani..shaurilako
wakichonga juu yako komaa nao atakayeona kabanwa atasogea..kazikaanga zitapomshindwa atatwanga abwie unga kautafuta umbea akubali na kusutwa...
ReplyDeleteMI SIJAELEWA HAPA
Delete