hili swala limekuwa kubwa sana katika ndoa zetu yano wewe kisa unamjuwa mume wa fulani au mkewe labda mlisoma wote au mlikuwa mnakaa wote kabla hajaoa ama kuolewa au labda mnafanya wote tu kazi basi unajifanya unamjuwa kuliko mama yake mzazi aliyemzaa na ndugu zake alionyonya nao ziwa moja.
Kuna jambo limetokea kwa watu ambao nilikuwa nawafahamu yani mpaka roho imeniuma, kuna wanandoa wanakaa mtaa wa nyuma wa nyumbani kwetu ni watu tu wa kawaida tu wanapenda kuongea na kuheshimu watu wote wa kubwa na wadogo, maisha yao ya kupendana sana kumbe yalikuwa yanawaumiza wa kina dada fulani ambao pia walikuwa wamepanga katika nyumba hiyo.
Yule baba kazi yake ni dereva wa malori ya kwenda congo, kama mnavyojuwa hawa wakirudi huwa wanafungasha sana kwa ajili ya familia yao kama ni mikaa, michele, na vipodozi matenge ya congo pc tatu ndio usiseme, kumbe yale yote yalikuwa yanawaumiza roho wakina fulani.
Basi huyu baba akarudi jumamosi ya juzi kutoka congo mkewe kampokea vizuri wakalala kesho yake yule mama akamuomba mumewe hela ya kwenda salon kutengeneza nywele kweli yule baba akampa na yule mama akaondoka kumbe bwana wale mashoga huku nyuma kugundua mwanamke ameenda salon maana aliwaaga nyumba za uswahilini jamani kama mmpepanga na hamna kazi kutwa huwa nje kwenye kibaraza wanasogoa na kutunga umbea..heri yako kama hujawahi kupanga hizi nyumba.
Wale wadada kuona hivyo wakajuwa wamepata pakumalizia shida zao, wakamsubiri yule baba akiwa anaelekea bafuni kuoga wakamsimamisha na kumueleza mambo mengi ya mkewe ananayoyafanya yeye akiwa safarini, na kwamba ana mwanaume na huko ndipo alipoenda sio salon, yule baba kwakweli mimi binafsi aliniudhi kwakuwa na roho ndogo kutomsubiri mkewe arudi hata wagombane kuhusu hayo maneno aliyoambiwa uamuzi aliouchukuwa ulisikitisha na bado watu wengi hawaamini.
Aliingia ndani akamuandikia mkewe baraua ya kwamba yeye alikuwa anampenda sana alikuwa akifanya kazi nzito zenye risk kubwa ili wapate kula na kutunza watoto wao ambao wangepata baadaye akifanya kazi kwa bidii akijuwa nyumbani kaacha mke kumbe yeye mkewe anafanya tu umalaya wa kuwa na wanaume wengi aksema limemuuma na hawezi kuvumilia akafunga kanga ya mkewe na kujinyonga mpaka kufa.
Mkewe aliporudi salon kuingia ndani anakutana na maiti ya mumewe ndio kuchanganyikiwa kupiga kelele watu kuja na kuanza kufanya mziba na gumzo kubwa mtaani, mkewe amechanganyikiwa baada ya watu kumpa ile barua ailyoiacha mumewe walipomsomea na kuanza kumuuliza alilia kwa uchungu na kusema toka niolewe sijawahi kumsaliti mume wangu na wala sikuwahi kufikiria akaanza kulia kwanini mumewe hakumsubiri amuulize ukweli akaamua kujiua ataenda wapi na atafanya nini kwakweli alilia kwa uchungu watu walisikitika sana.
wakati wanaenda kuzika wale wanawake waliomwambia mumewe umbea hawakuwepo katika kuzika wala msiba wote wapangaji wengine wakamalizia kwamba ni wao ndio waliongea hayo maneno japo mpaka leo wakiulizwa wanakataa ila kila mtu anasema ni wao.
Mmmeona vituko vya wakosaji, jamani ndoa sio nywele kila mtu anazo, na MUNGU naye anatujuwa mioyo yetu ndio maana wengine hawana ndoa wewe mwenyewe kujitunza huwezi utaweza kumtunza mume au mke..
MUNGU ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi...Amen
No comments:
Post a Comment