Emmanuel Kalema akiwa akimezungukwa na wananchi wenye hasira kali.
Wanandoa waliofarakana nchini Uganda wamewashangaza wakazi wa manispaa ya Nakawa, Kisenyi Zone.
Kulitokea
kutoelewana baina ya Emmanuel Kalema (32), na mkewe aliyefahamika kwa
jina moja la Aisha (28) hivyo mama huyo kuamua kufungasha vitu vyake na
kutaka kuondoka na watoto wao ndipo ghafla Kalema aliporopoka kuwa
akitaka kuondoka na watoto basi amchukuwe na Yule waliyemuua na kumzika
katika msingi wa nyumba yao iliyopo Kireka-Banda.
Maneno
hayo yaliushangaza umati uliokuwa ukishuhudia ugomvi huo hali
iliyopelekea watu kumzonga jamaa huyo na kumtaka atoe maelezo vizuri
kuhusiana na mauji hayo.
Akiwa
chini ya shinikizo la wananchi alisimulia kuwa yeye na mkewe
walishirikiana kumuua mtoto wa nje wa mama huyo na kumzika kwenye nyumba
hiyo ili waanze maisha mapya ya ndoa.
Baada
ya kupata taarifa hiyoi wananchi walichukua majembe na kuanza kuchimba
eneo lilitajwa na hatimaye walikuta mfuko wa plastiki ukiwa na mabaki ya
mtoto huyo.
Kalema yuko chini ya ulinzi wa polisi na uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea.
0 comments:
Post a Comment