Sunday, January 6, 2013

Dada Rose mimi ni msichana ambaye ninaishi na mwanaume kwa muda mrefu sasa, kabla hana kitu kabisa mpaka sasa amepata mengi na anaonekana wa maana akipita barabarani hata wanawake wengine kumtamani na kujiona yeye kidume.

Mwezi uliopita alirudi nyumbani akiwa amelewa mara simu yake ikaita alikuwa anaongea na mwanamke kwa mahaba tele wakati anajuwa ameshafika nyumbani, nilipoanza kumuhoji kwanini alikuwa anafanya hivyo tukaanza kugombana sana akawa ananiambia hii ni nyumba yake na kama naona anayofanya siyapendi niondoke.

Kwamaudhi na dharau zake kweli niliamua kupaki vitu vyangu nilichukuwa nguo zangu tu nakuondoka, nikarudi kwetu baada ya wiki tatu mwanaume wangu yule akaleta mwanamke nyumbani kwangu nakumbuka siku hiyo mdogo wake wa kiume alienda kumsalimia akamkuta huyo mwanamke ndio kunipigia na kuniambia nilipomuuliza kwani hakumuuliza kaka yake kwanini alileta mwanamke mwengine ndani akaniambia alipomuuliza alijibiwa ya kwamba kama mimi nimeshindwa basi wapo watakaoweza.

Mwezi ukakatika mimi nipo nyumbani kwetu na yeye anaishi na yule mwanamke wake, cha kushangaza nikawa nasikia kwa ndugu na majirani kwamba maisha yake siku hizi sio mazuri, kazi kafukuzwa yani kaishiwa amechakaa ukimuona huwezi kuamni kama ndio yule alivyokuwa zamani, nikawaambia hayo ndio maisha aliyoyataka.

Wiki iliyopita mara nikaona ananipigia simu nilishangaa kweli kuona simu yake akaniambia anataka kuja nyumbani kuongea na mimi pamoja na wazazi wangu, kwakuwa nilikuwa nampenda bado moyoni nikamruhusu aje  kweli siku hiyo akaja na ndugu zake kuomba msamaha yani japo nampenda lakini nilikuwa bado nahasira naye sana, akaomba kwa wazazi wangu wakanisihi nimsamehe, nami nikaamua kumsamehe.

Mimi na yeye hatujazaa bado japokuwa tumeshakaa wote kwa muda mrefu bado tunasubiri siku mungu atakapo tupa mtoto, akapangiwa siku aje kunichukuwa nyumbani, yani wanaume hawa hata mpaka anakuja kuomba msamaha kwetu yule mwanamke alikuwa hajamfukuza kwake, siku hiyo ndio tupo kwenye gari tunarudi namsikia anampigia simu kwamba uondoke mke wangu anarudi kwake nikija nisikukute.

Hata nguvu ya kugombana naye nilikuwa sina, tulipofika nyumbani nikamkuta yule mwanamke hayupo lakini vitu vyake bado vipo, majirani walifurahi sana kuniona basi wanawake wengi wakawa wanakuja kunipa na umbea siunaelewa sisi wanawake tulivyo mara baada ya lisaa limoja nikasikia hodi akaingia mwanamke mimi kwakuwa simjui nikamkaribisha vizuri akaingia akakaa ndio yule mwanaume kuniambia kwamba mwanamke mwenyewe ndio huyo.

Nilisikia chuki kunijaa moyoni lakini nikamuomba mungu anipe ujasiri, akaambiwa chukuwa vitu vyako akasema anataka apewe muda kidogo apumzike ndio aondoke mwanaume akagoma asipumzike mara yule mwanamke akajifanya anapandisha mashetani halafu yanaongea vibaya kuhusu mimi kwamba mimi ni mchawi na mambo mengine kibao yani aligaragara kama masaa manne basi watu kusikia maneno na makaelel wakajaa yani aibu anaongea maneno kibao kuhusu mimi naona mengi kayapata kutoka kwa mwanaume enzi zile mapenzi yamepamba moto, alikuwa akiongea mengi ya uongo lakini mengine ya ukweli.

Jamani nilipata aibu japo najuwa watu hawanauhakika kama ni ya kweli au la, ninachomshukuru mungu ni kwamba alinijibu maombi yangu na kunirudisha kwa mwanaume wangu japo mengi yametokea ndio tunapanga sasa kutaka kuoana maana nimemwambia sitaki kabisa kupotezewa muda na kudharauliwa kama mwanzo.

Kwanini nimekuandikia nataka wanawake wajifunze kutafuta ndoa na sio kuishi tu na wanaume maana wanaume bwana ukiishi naye bila ndoa anakuchukulia poa hajali wewe ni nani kwake ukitoka mwenzio anaingia kiurahisi maana hakuna kinachowaunganisha.

Ahsante

Teddy

1 comment:

  1. Dada teddy wewe una ndoa adi uwaambie wenzako wajifunze kutafuta ndoa nahisi ujitambui kama mwanaume tu huna nae ndoa unamwanika ivyo na umesema umemsamehe ukiwa na ndoa cndio utayaanika mengi wanawake mna mambo kwanza unajua nini maana ya mume wewe

    ReplyDelete