Tuesday, December 4, 2012

Ndoa hizi......

Jamani kwanza mimi naamini mwanamke yeyote sio mpaka awezeshwe ndio ayaweze haya maisha unaweza ukahangaika mwenyewe juu chini kwa njia za halali na zinazompendeza MUNGU huku ukimuomba kwa roho ya ukweli atakuinua tu, sio njia za mkato ili upate jambo ndio ujisifie kwamba umetoka na upo juu hapana.

Ndoa tunazitaka na kuzililia lakini je mnajuwa ya kwamba sio kila anyeamua kukuoa ama kuolewa na wewe anakupenda wengine wanakuja na mipango yao moyoni wengine wanataka kutoa nuksi kwao kwahiyo wanaolewa tu na ndio maana hawajali hata wakiachika baada ya mwezi.

Kuna wanaume wengine wanaoa kisa wameona mwanamke yule kwao ni matajiri kwahiyo wanatafuta njia za mkato za kupata mafanikio.

Kuna dada mmoja ameolewa na mzungu na kiumri wamepishana sana huyu dada ni mdogo sana kwa mumewe na MUNGU aliwapa utajiri kwakeli huyu mumewe ana kampuni moja kubwa sana na wanabonge la jumba na magari tele yani ni mwanamke ambaye ukipishana naye unaanza kwanza kujiangalia mara mbili maana ananukia pesa na utajiri.

Sijui ni matatizo gani waliyokuwa nayo ndani ya ndoa maana kuta zinaficha mengi na niwao tu wenyewe wanajuwa naona mdada kachoka akaamua kwenda kumchomea jamaa uhamiaji jamaa akafukuzwa ndani ya hiyo nchi masaa 24 na sirudi tena humo.

Lakini kama ninanvyosema huwezi juwa walikuwa na matatizo gani kabla hajafukuzwa muda fulani nyuma kumbe yule jamaa alibadilisha mali zake na kuandika jina na mtu mwengine ambaye hata mkewe hamjui ambaye hata mkewe hamjui mpaka magari na kampuni.

Yule mwanamke ndio kuhaha sasa kampuni na mali hana na mume pia hana alidhani kapata kumbe kapatikana.

Jamani tuweni makini na ndoa hii sio fashion na sio lazima kwamba kila mwanamke au mwanaume atembee na pete za ndoa mkono wa kushoto kama unaona bado hujapata ubavu wako subiri atakuja na labda hamna kabisa usijilazimishie hata kwenye bibilia imeandikwa kwamba kuna watu wataoa na kuolewa na wengine hawatakaa kuoa ama kuolewa labda na wewe ni mmoja wapo.

Kuwa na uhakika kwanza kabla hujamkubalia huyo unayetaka kumuoa/kuolewa naye.

No comments:

Post a Comment