Wapendwa kwanza kabisa nawaomba radhi kwa hii picha najuwa ni mbaya lakini nimeiweka hapo ili nifafanue jambo moja ambalo huwa tunafanya tunapowafumania wake/wame zetu kwa bahati mbaya au nzuri hii ndio niliyoipata ya hivi karibuni na bado kabisa sijapata ya wanaume kufumania wake zao mara nyingi kilio ni wanawake kufumania wame zao.
Jamani usiombe ukafumaniwa kwanza ni aibu kubwa na pili huyu aliyekufumania anaweza akakutoa roho maana hasira alizokuwa nazo kwa wakati huo sio ya kuchezea yani mtu unakuwa kama unalishetani limekupanda kichwani unalotaka wewe ndio ulifanye na hamna hata siku moja likakupanda lishetani ya kwamba umemfumania mkeo au mumeo umchukuwe kwa mapenzi umrudishe nyumbani muongelee umsamehe maisha yaendelee, wee thubutu yani tena pale kama ndio kuna kiti ama hata jiwe kama unaweza kubeba yani chochote kilichombele yako unabeba na kumtwanga mtu na mara nyingi sana huwa wanawake ndio wanaopata tabu yani unapigwa wewe mwanamke uliyefumaniwa na mume wa mtu lakini muewe anamuacha kabisa na wakifika nyumbani wengine wanamalizia huko ugomvi mwengine akishabembelezwa anamsamehe ila ushari na ugomvi bado unabaki kwa yule mwanamke atamtafuta tu bado na kumfundisha adabu.
Mwanamke na hapa nataka niongee na wake za watu sipendelei sana kuongea na watu ambao hawajaolewa ama kuoa kwasababu wao bado hawajaujuwa uchungu wa mume au mke yale maumivu yake ya ukweli yanayochanganya mpaka mara nyengine mpaka watu kuuwana bado hawajayajuwa ila ni vyema wakawa pia wanasoma wakajiandaa na habari nzima ya ndoa wakaelewa wanachokiombea ni nini.
Wewe kama mke wa mtu cha kwanza kabisa nataka ujuwe nafasi yako katika maisha ya mumeo ya kwamba mpaka mumeo amekuoa wewe alishakuwa na wanawake wengi sana kwanini akakuoa wewe??? kwanini MUNGU hakumpa mke mwengine na sisi wake tunawajuwa sana wanawake wa zamani wa wame zetu tena wengine ndio tukipishana nao tunawapa vikumbo mpaka wanajuta ukijitapa wewe ndio mkewe kakuacha wewe kanioa mimi sasa kwanini mwanamke ukitikiswa kidogo unayumbishwa?????
Jamani mwanamke ukiolewa na baadaye mumeo aitongozwe na kupendwa nje shoga kutunza mume bado hujajuwa labda urudi kwenu ukafundwe upya, hata kama akiwa ameokoka lakini kama ni mwanaume wa maana wanawake utaona tu wanajipitisha na kujigongesha mbele yake ilimradi tu wajitongozeshe sasa atakalofanya mumeo baada ya hapo ni kusudi lake..cha muhimu ni mwanamke umtunze mwanaume awe ng'aring'ari muda wote.
Unapomfumania mumeo kwamba anamwanamke iwe kwenye simu, au umemkuta live bila chenga shoga inauma lakini mwenzangu haiuhusu kuanza kujirusha roho kila mtu ajuwe kama umefumania malizana na mumeo chemba kwani wewe adhabu za wanawake huzijui ukawa unapayuka kama umemeza casset inahusu, wanaume hawapendi mwanamke mwenye maneno jamani wewe unapokuwa busy kumsema na kumpayaukia unampa nafasi ya kichwa chake kutokusikiliza wewe na kuwaza viuno alivyokuwa anapewa na huyo mwanamke unayemsema naye...hukujuwa chukua hilo
Kuna wanaake wengine washari jamani utapigiwa mpaka kigoma ukifumaniwa na mumewe na kutiwa aibu, lakini wewe mwanamke unapoenda na kumpiga na kumfanyia vituko huyo uliyemfumania na mumeo inasaidia nini??? kama uume kashaula kashaukatikia kashapewa raha kazikamua zote hata wewe nyumbani jana hukupewa sasa ukienda kumpiga na kumfanyia vurugu utarudisha yale masaa nyuma yale maraha aliyokuwa anampa mumeo uyarudishe kwa mumeo!!!!!
Unajitapa atanikoma atakukoma nini na upinde mpaka wa nyuzi za kutahiriwa mumeo anazijuwa unachotaka kufanya ugomvi naye ni nini kwani yeye alijipeleka mwenyewe sehemu ya tukio akamvuta mume kwa nguvu na kumbaka?????? shoga wa kumkomesha ni mumeo utamkomesha vipi sio kwa kumnyima unyumba, sio kwa kuhama chumba kisa umegundua ni malaya na wala sio kwakulala mzungu wa nne adhabu zote hizo bado zitamfanya atoke nje ya ndoa.
Kuliko kumnyima unyumba basi adhabu yake mpe lakini kwa condom hakuna adhabu mbaya wanaume wasioipenda kama kulala na mkewe kwa condom ni adhabu kwakwe lakini utakuwa unajikinga na maradhi mpaka hapo utakapogundua mumeo ametulia kwakuwa namwaambia wanaume hutumia condom kipindi cha kwanza wakishamzoea mwanamke hawavai condom hao asikudanganye analala nao na condom, sasa muendekeze mfe watoto wabaki yatima wakizurura barabarani wakati serikali inatafuta majibu ya kuwapunguza wewe ukaongeze na wakwako.
Akikuletea vurugu kashtaki kwa wakubwa, lakini imefuiika sehemu mwanamke ukajisimamia wewe mwenyewe ndoa nyingi wamama wameambukizwa ukimwi kwakushindwa kujisimamia wenyewe kwa kuwa wanaheshimu ndoa zao na wame zao lakini matokeo yake wameathirika na kupoteza maisha na kuacha watoto wakiteseka..Jitambue na chukua hatua sasa usiwe bendera fwata upepo.
No comments:
Post a Comment