STAA wa filamu aliyewahi kutamba na Kundi la Sanaa la Kaole la jijini Dar, Halima Yahaya ‘Davina’ Alhamisi iliyopita alifunga ndoa kimyakimya na mwanaume ambaye mpaka sasa hajaamua kumuweka hadharani, Ijumaa Wikienda linakujuza.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Davina alifunga ndoa hiyo bila ya wasanii wengi kujua na walipopata taarifa walipigwa na mshangao mkubwa.
Ijumaa Wikienda lilimtafuta Davina na kumuuliza kama ni kweli amefunga ndoa ambapo staa huyo alikiri na kusema kuwa wahudhuriaji walikuwa wachache kwa kuwa ndivyo walivyopanga.
“Walikuwepo ndugu na marafiki wa karibu, hata hivyo, maandalizi makubwa ya sherehe yanakuja, hivyo nadhani wengi nitawaambia,” alisema Davina.
Pia, Davina alifunguka kuhusiana na bifu lake na staa mwenzake Salama Salmin ‘Sandra’ na kusema msanii huyo anamchukia kwa kuwa alimkataza kuongea pembeni na mwanaume aliyefunga naye ndoa kipindi walipokuwa wachumba.
“Siku moja tulitoka na mchumba wangu (sasa mumewe) pamoja na Sandra ili kupata chakula cha jioni, Sandra akawa anataka kuongea pembeni na mchumba wangu jambo ambalo sikulipenda hata chembe, nikamkataza ndiyo akakasirika,” alisema Davina.
Staa huyo alisema kuwa siyo kweli kwamba Sandra ndiye alimuunganishia mwanaume huyo aliyefunga naye ndoa, bali alijuana naye tangu alipokuwa Kaole na mwanaume huyo akiwa nje ya nchi.
“Sandra alifanya jitihada nyingi kuweza kuharibu uhusiano wetu lakini imeshindikana, hicho ndicho chanzo cha ugomvi wetu,”alidai Davina.
No comments:
Post a Comment