Wednesday, November 7, 2012

Fumanizi......................

 Jamani kwanza naomba msamaha kwa mtu yoyote ambaye picha hii itamkwaza kwa namna moja ama nyengine lakini nimeshindwa kuvumilia lazima niiongelee hii picha na hii kitu ya kufumaniwa.

Katika mapenzi ni jukumu la kila mtu kumuheshimu mwenzake na kumjali na mpaka wewe unamuwa kuwa na huyo mpenzi wako inamaana umeona kati ya woote unaowaona mtaani hakuna aliyemfikia huyo ndio maana ukawa naye ama ukamuoa ama kuolewa, lakini wote tunatambua kama binadamu kunakupishana hapa na pale na kutoelewana sasa wewe unachukuliaje hizo hasira zako kwa mwenzako???

Tuseme leo kweli umemfumania kwani ukimfumania mwenzako ndio mwisho wa dunia???? mpaka ukamchoma mwenzako moto kisa umemfumania!! umeshajiuliza sababu zinazomfanya yeye atoke nje ya ndoa yake nini nini ama wewe kwasababu umemfumania unachukuwa jukumu kama hilo, wababa tafadhalini bwana.

Mwanaume yeye ukimfumania atakuomba tu msamaha na kukuambia shetani alinipitia huyo shetani anawaonaga nyie tu ila akimuona mkeo unamchoma moto jamani haipendezi, kama unaona mapenzi kati yenu hamna simuachane kama umemfumania na unajuwa mwenzio sio muaminifu kwanini usimuache ukatafuta mwengine huko nje wanaume na wanawake wapo kibao wameshushwa kwa vitabu chagua unayemtaka sio ung'ang'anie mwisho mkatoana roho.

Kuta zingekuwa zinaongea watu wasingekuwa na amani wanandoa wengi wanaishi pamoja kwasababu ya watoto tu utakuta mtu hata mapenzi hamna hata tunda hawachumi wanakaa tu kama kaka na dada ilimradi walee watoto wao hayo ndio maamuzi sahihi ya kufanya kama mmeona mmoja sio muaminifu lakini sio kuuana na kama wewe umemfumania mwenzio bora umwambia akuache kwa muda asirudi hata nyumbani hasira zitulie ndio muyaongelee maana ukiwa na hasira ndio mnaweza hata kutoana roho.

Jamani wewe ukimuona wa nini kuna mwenzako anawaza atampata lini, kama umechoka muachie mwenzio nafasi sio kumuharibu mtoto wa mtu hivyo ama kumtoa roho kama wewe umeshindwa kaa pembeni wanaojuwa kulea wakupokee..

Haipendezi kwakweli na imeniuma sana kumuona mwanamke mwenzangu amefanyiwa hivyo eti kisa amefumaniwa na mumewe..

No comments:

Post a Comment